Skip to main content

Posts

Showing posts from June 15, 2025

INSPEKTA KHALFAN, AWAHAKIKISHIA USALAMA WAJENZI KITUO CHA AFYA PANDANI

  NA KHAULAT SULEIMAN, PEMBA@@@@ MKAGUZI wa jeshi la Polisi shehia ya Pandani wilaya ya Wete, Khalfan Ali Ussi, aliwakikishia mafundi wanaojenga kiuto cha cha Pandani kuwa, kua jeshi la Polisi kwa kushirikiana ulinzi shirikishi, kitakua bega kwa bega, ili kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo bila ya uhalifu.   Alisema kua kazi ya jeshi la Polisi ni kuhakikisha usalama kwa wananchi wake, hivyo ni vyema kuendelea kufanya kazi zao wa weledi wa hali ya juu, na kujenga majengo yenye kiwango cha hali ya juu.   Mkaguzi huyo aliwataka wafanyakazi wa kampuni hiyo, kufanya kazi kwa uzalendo na uaminifu, ili kujali na kulinda maslahi ya ya taifa.   "Mkifanya hivyo mtaweza kujizuiya na matendo maovu, kama kujihusisha na vitendo vya udhalilishaji ikiwemo ubakaji, wizi, ulevi kwani jeshi la Polisi, halitosita kumchukulia hatua kali, kwa mfanyakazi yoyote atakaevunja sheria,"alisema.   Nae Mkandarasi wa ujenzi huo pamoja na msimamizi wa mradi huo Laurent...

MAHKAMA YAMUACHIA HURU ASKARI ALIYEDAIWA KUBAKA PEMBA

NA FATMA HAMAD, PEMBA@@@@ HATIMAE mtuhumiwa wa ubakaji wa mtoto wa miaka saba, ambaye ni Askari wa Jeshi la Polisi mwenye namba H.5290 D/C Godfrey Meckioru Mushi miaka (34)   wa   Limbani Wete, ameachiwa huru na mahkama ya mkoa iliyopo, Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba. Akitaja sababu za kuachiwa huru mtuhumiwa huyo Hakimu wa Mahkama hiyo Zuwena Mohamed Abdul-kadir alisema ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka, umekua dhaifu, na pia   umeshindwa kuleta mashahidi muhimu. Alisema jumla ya mashahidi wanne walisikilizwa, ingawa ushahidi wao haukuweza kuishawishi mahkama, na kuweza kumtia hatiani mtuhumiwa. Alisema upande wa mashataka hawakuleta shahidi ambae ni baba mzazi wa muathirika, ambae yeye ndie aliemuhoji na kumuambia kama, mtuhumiwa ndie aliemfanyia kitendo hicho. ‘’Mahkama imepata wasiwasi na ushahidi uliotolewa na mtoto mwenyewe, kwamba ni wa kupangwa,’’alieleza. Alifahamisha kwa kutokana na mazingita hayo, mahkama haikumtia hatiani, hivyo imemuachia hu...

MTUHUMIWA, WAKILI WAKE WAINGIA MITINI TUHUMA DAWA ZA KULEVYA

                                                            NA MARYAM SALIM, PEMBA@@@@ KUTOKUFIKA kwa mtuhumiwa Zaid Mussa Zaid miaka (46) mkaazi wa Machomanne pamoja na wakili wake katika mahakama ya Mkoa ‘C’ Chake Chake Pemba, kumepelekea shauri hilo kuahirishwa mahakamani hapo  na kupangwa tarehe nyengine kwa ajili ya utetezi .   Mapema Mwendesha mashitaka akiwakilisha Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka wa serikali, Kheir Hassan Omar, aliieleza mahkama hiyo mbele ya Hakimu Hamisuu Saadun Makanjira kwamba, shauri hilo lilifikishwa katika mahakama hiyo, kwa ajili ya utetezi ingawa mtuhumiwa na wakili wake, hawakuhudhuria.   "Mheshimiwa Hakimu, shauri lilimefikishwa mahakamani kwa ajili ya kusikilizwa utetezi, ambalo linamkabili mtuhumiwa Zaid Mussa Zaid, anaedaiwa kupatikana na dawa za kulevya.   "In...

MJIMBINI MKOANI MAJI 'FULL KUJIACHIA' WAIPA TANO ZAWA

  NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@ WANANCHI shehia ya Mjimbini wilaya ya Mkoani Pemba, wameipongeza Serikali kupitia Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), kwa upatikanaji wa maji safi na salama shehiani mwao. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Juni 20, 2025 mwananchi   Saumu Issa Mohamed alisema, huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama kijijini hapo, kwa sasa ni yauhakika jambo linalotoa faraja kwao. Alisema mafanikio hayo ni muhimu kwao, kutokana na umuhimu wa huduma hiyo katika maisha yao ya kila siku, hivyo wameipongeza serikali kwa kuwahakikishia   upatikanaji wa huduma hio saa ishirini na nne. Mwananchi Suleiman Muhammed Makame kutoka shehiani hapo alisema, kwa miaka zaidi ya saba iliopita,   iliwalazimu kutumia maji ya mito na visima ambayo hayakua safi na salama, kwa matumizi ya binaadamu, hivyo upatikanaji wa huduma hiyo imekua suluhu ya tatizo   hilo. Nao Zahra Hafidh Juma na Hafidh Khatib Faki, walisema, upatikanaji wa huduma hio ni utekelez...

MAJIMBO YA UCHAGUZI CHINA HAYASHIKIKI KWA WANAWAKE, RAIS WAO AENDELEA KUWEKA MAZINGIRA RAFIKI

  NA HAJI NASSOR NIPO, jiji la Beijing linalopatikana takriban saa 12, kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zanzibar, kwa usafiri wa anga. Jiji hili ni moja kati ya majiji manne yayounda taifa la China, likiwemo pia lile la Shanghai, ingawa Beijing ndio mji mkuu. Lenyewe limezungurukwa na milima mikubwa kwa upande wa magaribi, ingawa kusini mashariki na kaskazini mwa jiji hilo, linaujirani na bahari iitwayo Bohai. Jiji hili, lina ukubwa wa skweya kilomita 16,410, ambapo hadi mwishoni mwa mwaka 2023, lilikuwa na wakaazi milioni 21.858. Kati yao hao, wanaoishi ndani ya mji husika wa kudumu ni watu milioni 19.198, sawa na asilimia 87.8, huku ambao sio wa waakzi wa kudumu ni milioni 8.204 sawa na asilimia 12.2. Mpaka mwezi April 2023, Beijing pekee inazo wilaya 16 ‘ municipal districs’ ikiwemo ya Xichenga, Chaoyang, Fengatai, Shijingshan, Hiaidian, Miyun pamoja na wilaya ya Yanging.    Ukingia ndani ya jiji la Beijing, mara zote utakaribishwa na mazingira maz...

MICHEWENI WAONYESHWA NJIA KUEPUKA MATUMBO YA KUHARISHA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI wa Halmashauri ya wilaya ya Micheweni Pemba, wametakiwa kurejea utamaduni wao wa kuweka mazingira yao safi na salama, ili kujikinga na magonjwa ya kuharisha, ambayo chanzo chake kikuu ni uchafu. Ushauri huo umetolewa jana na Mwanasheria wa Halmashauri hiyo, Rukia Khamis Haji, alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hii, kufuatia uwepo wa tishio la matumbo ya kuharisha, katika baadhi ya maeneo kisiwani Pemba. Alisema, suala la usafi haipendezi kuona wananchi wanalifanya kwa shindikizo la Halmshauri, bali wenyewe waamue kujielekeza kwenye usafi, ili kujihakikisha usalama wao. Alieleza kuwa, utamaduni wa kuweka mazingira safi na salama, ni vyema kwa wananchi wa Halmashauri hiyo, ikawa ndio utamaduni wao endelevu, kwani kinyume chake ni kujiangamiza. ‘’Hichi ni kipindi cha mvua na kinakuwa na changamoto zake, ikiwemo kusambaa kwa uchafu kutoka sehemu moja kwenda nyingine, hivyo suala la usafi lazima liwe kipaumbele chetu,’’alieleza. ...

RC SALAMA: AKABIDHIWA RIPOTI YA AWALI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ IDARA ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar, imemkabidhi ripoti ya awali, ya kampeni ya msaada wakisheria ya Mama Samia, mara baada ya kumalizika kwa kambi ya siku 10 ndani ya mkoa huo. Kabla ya kukabidhi kwa ripoti hiyo, Mkuu wa Idara hiyo Pemba Bakari Omar Ali, alipongeza ushirikiano alioupata kutoka kwa maafisa wa taasisi mbali mbali za serikali, wakati wote wa kampeni hiyo. Alisema, katika kampeni hiyo, waliwatumia maafisa wa kamisheni ya wakfu, ardhi, mawakili wa serikali, makadhi, maafisa ustawi, matukio ya kijamii pamoja na waandishi wa habari. Alieleza kuwa, maafisa hao walisaidia kwa kiasi kikubwa, kupokea malalamiko na kuyapatia ufumbuzi papo hapo na mingine kuziandikia barua taasisi husika. Alifahamisha kuwa, kampeni hiyo ambayo ilikuwa katika mifumo miwili, moja ni kuwafuata wanafunzi wa skuli, vyuo vya elimu ya juu pamoja na mikutano ya jamii. ‘’Tulijigawa timu mbili, moja wilaya ya Micheweni na nyingine Wete, ambapo maafisa k...

WALIOBAKA KWA KUNDI PEMBA ADHABU YAO HII HAPA

    NA FATMA HAMAD, PEMBA@@@@ KIVUMBI na vilio viliibuka katika Mahkama ya mkoa Wete, kufuatia washitakiwa Suleiman Said Khamis (19) na Ali Iddi Ali (33) kwa kutaka kujitupa dirishani, baada ya kupelekwa Chuo cha Mafunzo kwa muda wa miaka saba, na kulipa fidia ya shilingi milioni 1, kwa kila mmoja kwa kosa la kubaka kwa kikundi.   Kabla ya kusoma hukumu yao jana Juni 17, 2025, Hakimu wa Mahkama hiyo Zuwena Mohamed Abdulkadir, alisema jumla ya mashahidi sita walisikilizwa mahkamani hapo, na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka haukuacha chembe ya shaka na umewatia hatiani.   "Kutokana na ushahidi uliotolewa na mashidi wetu, mahkama tumeridhika na kwani hauna chembe ya shaka,"alisema.   Alisema kwa mujibu wa vifungu cha 108(1) na 110 (1), (2) vya vheria namba 6 ya mwaka 2018, kinaeleza kwamba kosa, la kubaka kwa kikundi adhabu yake ni kifungo cha maisha.   Kabla ya kutolewa hukumu hiyo Mwendesha Mashtaka wa serikali Juma Mussa Om...

DK. MWINYI ASEMA JUKWAA LA UWEKEZAJI LA MWAKA 2025, KUWAVUTIA WAWEKEZAJI PEMBA

    NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema jukwaa la uwekezaji la mwaka 2025, litakuwa chanzo kikubwa cha kuwavuta uwekezaji, kutoka maeneo mbali mbali ulimwenguni, kuekeza Pemba. Dk. Mwinyi aliyasema hayo jana, kwenye jukwaa la uwekezaji, wakati akizungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari, lililofanyika maeneo huru ya uwekezaji wilaya ya Micheweni kisiwani humo. Alisema, anaamini baada ya jukwaa hilo kumalizika, sasa wawekezaji watamiminika kisiwani, na hasa kwa vile katike maeneo hayo huru, yapo miundombinu rafiki kwa ajili yao. Alieleza kuwa, jukwaa hilo sasa litachapuza maendeleo ya haraka ya kisiwa hicho, kama ilivyo kwa Unguja, hasa kwa vile ujenzi wa barabara kadhaa, unaendelea kwa kasi na zipo ambazo zimeshakamilika kwa kiwango cha lami. Dk. Mwinyi alisema, hata ujenzi wa bandari za Mkoani Pemba, imeshatanuliwa na huku ujenzi wa bandari ya Shumba ukiendelea, kama ambavyo wakati wow...

MHANDISI ZENA AONGOZA MATEMBEZI JUKWAA LA UWEKEZAJI LA MWAKA 2025 PEMBA, AWAAMSHA WANANCHI

    NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ KATIBU wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, amesema tayari serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imeanza kwa vitendo kukifungua kisiwa cha Pemba kiuchumi. Mhandisi Zena aliyasema hayo jana, eneo huru la Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba, mara baada ya kuyapokea matembezi ya wanavikundi vya mazoezi na wananchi, kwenye kongamano la uwekezaji la mwaka 2025, yalioandaliwa na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar ‘ZIPA’. Alisema, kufanyika kwa kongamano hilo ni sehemu ya kukifungua kisiwa hicho kiuchumi, ujenzi wa barabara kadhaa za kisasa pamoja na utanuzi na ujenzi wa bandari mbali mbali. Alisema, serikali inayoongozwa na Dk. Hussein Ali Mwinyi, inaendelea kuonyesha kwa vitendo nia yake ya kukifungua kisiwa cha Pemba, kama alivyokuwa akiinadi wakati wakati wa kampeni. Alieleza kuwa, kilichobakia kwa wananchi wa Pemba, ni kushirikiana kwa karibu na serikali yao, ambayo ina nia ya dhati kuona uchumi wa Pemba, u...