NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAWAKE wa shehia wa Makombeni wilaya ya Mkoani Pemba, wameomba kuongezewa ufahamu juu ya dhana ya uchumi wa buluu, ili waifahamu kwa kina malengo ya serikali kuu. Walisema, wamekuwa wakisikia juu juu ya dhana hiyo, ingawa bado wamekuwa hawana uwelewa wa ndani, na kusababisha kubakia na uwelewa wa wao zamani. Wakizungumza na waandishi wa habari wa Shirika la Magazeti ya serikali Zanzibar ofisi ya Pemba waliofika kusikiliza changamoto zao, walisema bado dhana hiyo haiku vyema kwenye akili yao. Walisema kua, wanahitaji mamla husika kufika Makombeni kuwaeleza kwa kina juu ya dhana ya uchumi wa buluu, ili waende samba mba na kaluli ya rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi. Mmoja kati ya wanawake hao Mayasa Makame Chumu, alisema bado baadhi yao wamekuwa wakisikiliza vyombo vya habari, ingawa dhana hiyo bado hawajaipata vyema. ‘’Dhana ya uchumi wa buluu tunaiskia kwenye vyombo ya habari, lakini hasa ku...