IMEANDIKWA NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ UZAZI wa mpango ni suala lenye kuleta utata kwa baadhi ya wanajamii ambalo huchukuliwa kwa sura tofauti. Kwani kuna baadhi yao huamini kwamba, uzazi wa mpango ni kufunga kizazi moja kwa moja, jambo ambalo sio sahihi, kwa sababu ni sawa tu na kusema... ‘kumuachisha mtoto’. Na kuachishwa mtoto ni kumpa nafasi mama aliejifungua kupumzika kwa ajili ya kuimarisha afya yake na mtoto, hivyo ni sawa na uzazi wa mpango. Jamii ifahamu kwamba kutumia uzazi wa mpango ni muhimu sana katika kuimarisha afya za akinamama na watoto, kwani dini ya kiislamu imehimiza mtoto kunyonyeshwa miaka miwili. Qur-an tukufu katika Suratul-Baqara aya ya 233 imeeleza kuwa, ‘Wazazi wa kike wanyonyeshe watoto wao miaka miwili kwa mwenye kutaka kutimiza kunyonyesha…’ Hiyo inaonesha wazi kwamba, kuachisha mtoto kwa miaka miwili ni muhimu sana kwa akinamama kutokana na faida inayopatikana ndani yake. Lakini kuna baadhi ya akinababa huipa kisogo aya hiyo na kuamua ...