NA NAFDA HINDI, ZANZIBAR@@@@ Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa habari Wanawake Tanzania Zanzibar Dk Mzuri Issa amesema kuwepo kwa Sheria mpya ya habari inayokwenda sambamba na maendeleo ya Sayansi na teknolojia itatowa fursa kwa waandishi wahabari kufanya kazi zao kwa ufanisi. Akitowa taarifa kwa vyombo vya habari amesema pamoja na kuwepo maoni mengi yaliyotolewa na waandishi wahabari pamoja na wadau na watetezi wa haki za binadamu kuhusu mabadiliko ya sheria ya zamani iliodumu kwa takribani muongo mmoja bado kunahitajika kuwepo kwa sheria rafiki inayokwenda na wakati wa sasa. Dk Mzuri amewapongeza wadau mbali mbali walioshirikiana na vyombo vya habari ikiwemo Serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata haki yao ya msingi ya kupata habari kama inavyosema Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu cha 18, pamoja na Mikataba ya Kikanda inayosimamia uhuru wa vyombo vya habari nchini. “Wakati tunaingia mwaka mpya 2024 waandishi na vyombo vya habari wana matumaini makubwa ya kuzita...