NA HAJI NASSOR, UNGUJA::: WANANCHI laki 118,760 wakiwemo wanawake 60,203, wanaume 39,641 na watoto 18, 232 wamenufaika na elimu, msaada na ushauri wa kisheria kwa muda wa miaka 30 na kati ya hao, laki 108, 860 wameshinda kesi na kupata haki zao mbali mbali. Aidha kati ya hao 11, 8760 ni wananchi 9, 216 pekee ndio ambao licha ya kupata elimu na msaada huo wa kisheria, walishindwa katika kesi zao . Akizungumza kwenye kongamano la maadhimisho ya siku ya haki za binaadamu duniani, leo Disemba 10, 2022 lililofanyika Kijangwani mjini Unguja, na kuandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar 'ZLSC' kwa kushirikiana na Tume ya Haki za Binaadamu 'CHRAGG' kwa ufadhili wa Umoja wa Mataifa, Ofisi ya Haki za Binaadamu 'UN-OHCHR' Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho Harusi Miraji Mpatani, amesema wastan kwa mwaka waliopatiwa msaada ni wananchi 3, 936. Ameeleza pia Kituo kiliwasaidia watoto na masuala ya kisheria 18,232, ambapo pia kwa upande mwengine, Kituo hicho ...