Skip to main content

Posts

Showing posts with the label SHERIA

WANANCHI KASKAZINI PEMBA, ZITUMIENI SIKU 3 ZA KAMBI YA KISHERIA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI wa mkoa wa kaskazini Pemba, wametakiwa kuzitumia siku tatu za kambi ya kutoa masaada wa kisheria, ili kufikisha malalamiko yao ya kisheria, na kupatiwa ufumbuzi papo hapo. Hayo yameelezwa leo Oktoba 17, 2024 na Mkuu wa mkoa wa kusini Pemba Mattar Zahor Massoud, katika hutuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya ya Wete Dk. Hamad Omar Bakari, kwenye uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia, iliyozinduliwa uwanja wa Majengo Micheweni Pemba. Alisema, siku tatu hizo watakuwepo wanasheria, Jeshi la Polisi, wasaidizi wa sheria, mahakim na mawakili, ili kusikiliza changamoto za kisheria na kuzitolea ufumbuzi papo hapo. Alieleza kuwa, kuwapata wanasheria wakati mwingine huwa ni vigumu, ingawa kufuatia uzinduzi wa kampeni hiyo, wanapatikana papo hapo bila ya malipo. ‘’Niwatake wananchi wa mkoa wa kaskazini Pemba na hasa wa wilaya ya Micheweni, kufika hapa Micheweni majengo, ili kupata elimu na msaada wa kisheria tena ...

DC.MJAJA: ‘UHURU WA KUJIELEZA UNAMIPAKA YAKE’

    NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MKUU wa wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja, amesema ni lazima waandishi wa habari, wanasiasa na wanaasasi za kiraia, kuutumia vyema uhuru wa kujieleza, ili kuepusha madhara yanaoweza kujitokeza. Kauli hiyo ameitoa, ukumbi wa Chuo cha Samail Gombani Chake chake Pemba, wakati akifungua semina ya kijamii, kuhusiana na uhuru wa kujieleza, iliyoandaliwa na Jumuiya ya Waandishi wa habari Pemba ‘PPC’ kwa kushirikiana na Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania ‘UTPC’ na kuwashirikishi waandishi wa habari, wanasiasa, jamii na viongozi wa dini. Alisema, ni kweli uhuru wa kujieleza ni haki ya kikatiba, na nivigumu mtu kumzuia kutoitumia haki hiyo, ingawa suala la tahadhari ya kukiuka mipaka, ni jambo la kuzingatia. Alieleza kuwa, waandishi wa habari hutumia vyombo vya habari kama tv, redio, magazeti na vile vya mtandaoni, ili kufikisha ujumbe kwa jamii husika. ‘’Hapa kwa eneo hilo, la kuzingatia zaidi ni, ili kuepusha machafuko ni kuhakikisha habari...