Skip to main content

Posts

Showing posts from May 10, 2026
  TAMWA - ZANZIBAR YAWAPIGA MSASA WAANDISHI KUTIPOTI HABARI ZA UDHALILISHAJI MAENEO YASIO RASMI   NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@ MRATIBU wa Program ya Mradi wa kupambana na vitendo vya udhalilishaji wa "Tunaweza kwa pamoja   kutokomeza vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia" kwa wanawake na wasichana unaotekelezwa na   chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA -ZANZIBAR   kwa kushirikiana na UN - WOMEN, Asia Hakim Makame amewataka waandishi wa habari kutumia taaluma zao kuielimisha jamii juu ya masuali mbali mbali ya udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na wasichana. Alisema waandishi wa habari wanamchango mkubwa katika kutoa elumu ya kupinga vitendo vya udalilishaji wa kijinsia   kwa wanawake na watoto hususan katika sekta zisizo rasmini ikiwemo ya uchumi,elimu, afya na usafirishaji. Aliyasema hayo wakati   akifungua mafunzo ya uandishi wa habari hizo yaliojumuisha waandishi kutoka vyombo mbali mbali vya habari watakao tekeleza mradi huo ...

‘WEPO’ YAMALIZA MRADI KWA MAFANIKIO MAKUBWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI 710, wakiwemo wanafunzi wa kike 663, sambamba na wasikilizaji 4,800 wa redio mbalimbali, wamefikiwa na elimu ya kisheria, haki za binaadamu, kupitia mradi uliokuwa ukiendeshwa na Jumuiya ya wasaidizi wa sheria Wete ‘WEPO’ hivi karibuni. Hayo yalibainishwa na Mratibu wa Uwezeshaji wa upatikanaji wa haki, kutoka ‘WEPO’ Rashid Hassan Mshamata leo Mei 10, 2026 skuli ya sekondari ya Utaani Wete, wakati wa mjadala wa wazi. Alisema, wapo waalimu na wazazi, wakimwemo wanawake 27 na wanaume 19, walifikia wakati wa utekelezaji wa mradi huo. Alieleza kuwa, kwa sasa matumaini yao, ni kuona jamii, imebadilika na waliokalia haki za wingine, sasa wanapata haki zao, kama sheria zilivyo. Alifafanua kuwa, kwa mfano waligundua ipo familia, ambayo, haijarithi kwa miaka 30 sasa, ambapo wanaume, wamekalia mirathi, jambo ambalo linaendelea kuwanyima haki wingine. ‘’Mradi huu, tulifanya shughuli kadhaa, lakini mafanikio yapo, maana hata wakati wa urushaji ...