Skip to main content

Posts

Showing posts with the label UDHALILISHAJI

ALI MBAROUK WA KONDE KUUKARIBISHA MWAKA MPYA AKIWA CHUO CHA MAFUNZO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ HAKIMU wa Mahkama ya Mkoa Wete, Zuwena Mohamed Abdul-kadir, amemuhukumu kwenda chuo cha mafunzo kwa kipindi cha miaka minne, mshitakiwa Ali Mbarouk Suleiman mwenye (18) mkaazi wa Konde Chanjaani, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kuvunja nymba usiku na kuiba. Mshitakiwa huyo ametiwa hatiani kwa makosa ya kuvunja nyumba na kuiba Simu moja aina ya Sumsung, yenye thamani ya shilingi 138,000 kwa kukisia mali ya Said Mohamed Salim. Aidha Hakimu huyo alieleza kuwa kosa la kwanza la kuvunja nyumba usiku atatumikia  chuo cha mafunzo kwa muda wa mika mitatu, na kosa la pili la kuiba simu atumikia kwa muda wa mwaka mmoja. Mbali na adhabu hiyo, pia alitoa agizo la kurejeshwa simu kwa mmiliki ambapo, hapo awali wakati wa kuiendesha kaesi hiyo, ilikua ni kielelezo cha ushahidi mahkamani hapo.  Mwendesha Mashtaka wa serikali Mohamed Ali Juma, alieleza kuwa kwa vile Mahkama imemuona na hatia mshitakiwa huyo, ni vyema kutoa adha...

ZAFELA YAZINDUA KAMPENI SIKU 16 PEMBA, YATOA UJUMBE MZITO

  NA KHAULAT SULEIMAN, PEMBA@@@@ MWENYEKITI  wa Chama cha Wanasheria wanawake Zanzibar, 'ZAFELA' Hamisa Mmanga Makame, ameiomba jamii kuchukuwa hatua dhidi ya kupiga udhalilishaji wa kijinsia nchini kwa wanawake na watoto.  Ameleza hayo leo Novemba 26, 2024 katika uzinduzi wa  kampeni ya  siku 16 za kupiga udhalilishaji wa kijinsia yaliyofanyika katika uwanja wa Majenzi wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba.   "Kujitokeza kwa wingi ili kupinga udhalilishaji na kupata elimu ya udhalilishaji kutoka ZAFELA na kuwahamasisha na wingine ili matendo ya udhalishaji yaweze kuondoka.  Mapema Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib, amewataka wananchi kutoa ushirikiano pindi tu inapotokea vitendo hivyo, ili sheria kuchukuwa hatua kali kwa mtuhumiwa wa makosa hayo.  Aidha alizishukuru tasisi na jumuiya za asasi binafsi na za kiserekali ambazo zina lengo la kupinga na kupeleka ujumbe katika jamii, ili kupambana na vitendo vya udhalilishaji ...

SAADA MKUYA AZINDUA SIKU 16 ZA KUPINGA UDHALILISHAJI, ATOA NENO

  HOTUBA YA MHE. DR. SAADA MKUYA SALUM WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS FEDHA NA MIPANGO KATIKA UZINDUZI WA SIKU 16 ZA HARAKATI ZA KUPINGA UDHALILISHAJI WA KIJINSIA, KATIKA UKUMBI WA CHUO CHA POLISI ZANZIBAR WILAYA YA MJINI MKOA WA MJINI MAGHARIBI -UNGUJA.  TAREHE 25/11/2024.   MHE. RIZIKI PEMBE JUMA,WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO. MHE. ANNA ATHANUS PAUL, NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WAZEE NA WATOTO, MHESHIMIWA IDRISA KITWANA MUSTAFA, MKUU WA MKOA M/MAGHARIBI, NDUGU KHATIB MWADINI, KAIMU KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAEDNELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO, MUWAKILISHI WA SHIRIKA LA UN WOMEN, MWAKILISHI WA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA IDADI YA WATU DUNIANI (UNFPA) ZANZIBAR, WAHESHIMIWA WAKUU WA WILAYA MLIOPO, NDUGU HAFIDH ALI, AFISA MDHAMINI WMJJWW, WAKURUGENZI MBALI MBALI MLIOPO, MAOFISA KUTOKA WIZARA NA MASHIRIKA MBALI MBALI, WARATIBU WA WANAWAKE NA WATOTO, WANAHARAKATI MBALIMBALI MLIOPO, NDUGU WAANDISHI WA HABARI , NDUGU WAALIK...

WAZIRI PEMBE ATOA TAARIFA KWA WAANDISHI KUELEKEA SIKU 16 ZA KUPINGA UDHALILISHAJI

  HOTUBA YA MHE. RIZIKI PEMBE JUMA WAZIRI WA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO KWA WAANDISHI WA HABARI KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA HARAKATI ZA KUPINGA UKATILI NA UDHALILISHAJI WA KIJINSIA, KATIKA UKUMBI WA WIZARA, KINAZINI MKOA WA MJINI MAGHARIBI,  TAREHE 21/11/2024.   ·  MHE. ANNA ATHANUS PAUL, NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WAZEE NA WATOTO, ·  NDUGU MWADINI KHATIB MWADINI, KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA  WAZEE NA WATOTO, ·  NDUGU WAKURUGENZI WOTE, ·  WAANDISHI WA HABARI ,   ASSALAAMU ALAYKUM.  Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema  kutujaalia uzima na afya njema na kutuwezesha kukutana hapa tukiwa wazima wa afya, kwa lengo la kuzungumza nanyi kuhusu siku 16 za mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili na Udhalilishaji tuseme Alhamdulillah. Kwa kipekee napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza ...

WANAUME WANAOPIGWA NA WANAWAKE CHAKE CHAKE WATAKA DAWATI KUTOA MALALAMIKO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAUME wa shehia za Kibokoni na Vitongoji wialaya ya Chake chake, wamesema wakati umefika sasa, wa kuanzishwa kwa dawati la siri la kundi lao, ili kutoa malalamiko, wanapopewa kichapo na wanawake. Ushauri huo wameutoa Septemba 5, 2024 kwenye kongamano la kujadili njia za kutokomeza ukatili na udhalilishahaji wa kijinsia, lililoandaliwa na Mwemvuli wa asasi za kiraia Pemba ‘PACSO’ na kufanyika skuli ya sekondari ya Vitongoji wilayani humo. Walisema wapo baadhi yao, wanaopokea vipigo kutoka kwa wake zao, ingawa wamekuwa hawajui wapi wakaripoti madhila hayo. Walieleza kuwa, wapo wanawake wamekuwa wakatili kwa waume zao, ingawa wanapokumbumbwa na changamoto hizo, hushindwa wapi wakaripoti. Mmoja kati ya wanaume hao, Salim Ayoub, alisema wanaoa aibu kwenda moja kwa moja kituo cha Polisi kuripoti matukio hayo, hivyo kama wataanzishiwa dawati lao, watejenga uthubutu wa kuziripoti kesi hizo. Alifahamisha kuwa, kama serikali inataka kujua njia sahih...