Skip to main content

Posts

Showing posts from May 18, 2025

MAUWAJI CHAKE CHAKE YAACHA SIMANZI: WANANCHI WASUBIRI KWA HAMU UPELELEZI POLISI

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI wa shehia ya Mgogoni wilaya ya Chake chake, wameliomba Jeshi la Polisi mkoa wa kusini Pemba, kuharakisha upelelezi wao, ili kumbaini mtu aliyedaiwa kumbaka na kisha kumuua mwanamke mmoja wa kijiji hicho mwenye miaka 55. Wananchi hao walisema, kitendo alichitendewa mwananchi mwenzao, sio cha kiungwana na kinafaa kulaaniwa na kila mmoja, na kuliomba Jeshi la Polisi kuharakisha upelelezi wao. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, walisema wanasikitishwa mno na mzazi mwenzao, kufanyiwa kitendo hicho na kisha mwili wake, ukiwa hauna nguo kutelekezwa kichakani. Mmoja kati ya wananchi hao, Mohamed Juma Maalim, alisema kilichobakia kwa sasa pamoja na kushirikiana na Jeshi la Polisi, lakini wanalisubiri kuona upelelezi wao unazaa matunda gani. “Ni kitendo kinachoumiza hadi ndani ya miili yetu, kuona mtu aliyefanya kitendo hicho, hakuishia tu kwenye kumdhalilisha kingono, lakini kisha kuondoa uhai wake,’’alisema. Nae Khadija Mjaka Makame, alisema wali...

WAANDISHI WA HABARI: 'CHINA ITOWE MISAADA MIKUBWA KWA AFRIKA IJITEGEMEE'

    NA HAJI NASSOR, ALIPOKUWA BEIJING WAANDISHI wa habari wa mataifa ya Afrika, wameiomba serikali ya China, kuyapa mataifa yao miradi endelevu mikubwa ya maendeleo, ili baadae yaweze kujiendesha, badala ya kutegemea misaada kila baada ya muda. Wakizungumza kwenye ziara ya kuvitembelea vituo vya Tehema, star times vilivyopo Beijing nchini China, walisema urafiki na uhusiano wa China na mataifa ya Afrika, unaweza kuchapuzwa na miradi mikubwa. Mwandishi wa habari kutoka Gambia Arret Jatta, alisema kwa muda mrefu mataifa hayo, yamekuwa yakipokea misaada kutoka kwa serikali ya China, ingawa baada ya miradi kumazilika, hurejea kwenye utegemezi. Alieleza kuwa, China imekuwa ikitumia mamiliobi ya dola, kuyaunga mkono mataifa ya Afrika, ingawa huwa ni kwa kiasai kidogo, kwa mujibu wa mahitaji ya wakati uliopo. ‘’Wakati umefika sasa kwa taifa la China, kulielekea taifa moja moja la Afrika, na kulipa msaada mkubwa wa maendeleo, katika nyanja ama ya elimu, afya, miundombinu ili...