Skip to main content

Posts

Showing posts from October 11, 2026

‘RESI’ ZA NGALAWA MANAHOZA WAMBAA, MAKOMBENI, MAKOONGWE WAZAA 'DABI'

    NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@ NGALAWA ni usafiri ambao wazee wa zamani, waliutumia kwa ajili ya safari zao, hasa kwa shughuli za kibiashara na uvuvi. Usafiri huu ni urithi wa utamaduni wa mzanzibari, ulioanza kutumika katika miongo iliopita, ingawa hadi sasa hutumiwa, lakini sio sana kama ilivyokua hapo zamani. Hili limepelekea kuchukuliwa kama moja ya urithi mkubwa wa kihistoria kwa waswahili wa Zanzibar na wale wa ukanda wa pwani. Ndio maana, katika matamasha mbalimbali ya utamaduni wa Zanzibar, ngalawa zimekua sehemu muhimu ya matamasha hayo na kua kivutio kikubwa kwa hadhira. Kwani hadhira kubwa ya watu ambao huenda katika matamasha hayo, hufurahia kuona jinsi watu wanavyoendeleza utamaduni huo, ambapo huko hufanyika mashindano ya resi za ngalawa. Septemba 21, mwaka huu ilikuwa ni siku ya pili ya tamasha la 31 la utamaduni wa mzanzibari, tokea kufunguliwa kwake Septemba 19, ilikua ni siku ya kukumbuka urithi wa utamaduni wa kuendesha ngalawa. Utamaduni a...

MCHEZO WA NG’OMBE PEMBA, UTAMADUNI UNAOBEBA WASHABIKI WINGI

                                  NA MARYAM SALUM, PEMBA@@@@   KELELE za watazamaji, mlio ya zumari, ukichombozwa na ngoma za asili, ndizo zinazoteka nyonyo za wapenzi wingi wa mchezo wa Ng’ombe, baada ya mpira wa miguu.   Mchezo huu ambao umejengeka katika historia ya   maisha ya jamii ya Pemba, si burudani pekee, bali ni sehemu ya urithi wa kitamaduni unaounganisha vizazi vya zamani sasa.   Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali kuhusu historia ya mchezo huo, asili yake Pemba imehusishwa na mwingiliano wa kihistoria, kati ya jamii za Pemba na Wareno.     Baadhi ya vyanzo vinaeleza kuwa, mchezo huo uliingia katika visiwa hivyo kupitia Wareno, ingawa simulizi za wenyeji pia, zimekuwa zikihifadhi historia yake, kutoka kizazi hadi kizazi.   Akizungumza, katika mchezo wa Ng’ombe uliofanyika uwanja cha Pujini wilaya ya Mkoani, Wazir...