NA HAJI NASSOR, PEMBA WATAALAMU wa sheria Zanzibar, wameitaka Idara ya Katiba na Msaada wa sheria Zanzibar, kuongeza jitihada za elimu ili kusaidia kubadili mawazo, mitazamo na uwelewa wa watu maskini, ili kuongeza matumizi ya huduma za msaada wa kisheria. Walisema, Idara inapaswa kuweka kipaumbele cha pekee cha kutoa mafunzo hayo, ili kuona walengwa wa mfumo wa kutoa elimu, ushauri na msaada wa kisheria ambao ni watu maskini wanafaidika nao. Kwa mujibu wa tafsiri ya ripoti ya tathmini ya awali ya hali halisi ya msaada wa kisheria Zanzibar ya mwaka 2020, iliyotolewa na wizara ya Katiba na sheria, walisema azma ya uwepo wa msaada wa kisheria ni kwa watu wasio na uwezo. Wataalamu hao kwenye ripoti hiyo walisema, suala la utoaji wa msaada wa kisheria linazingatiwa kuwa ni miongoni mwa viashiria vya msingi ya upatikanaji haki. Walieleza kuwa, taifa lo...