NA NUSURA SHAABAN, ZANZIBAR@@@@ KATIKA dunia ya leo, umuhimu wa kuwaandaa watotowa kike kuwa viongozi wa kesho hauwezi kupuuzwa, Skulini ndiko safari ya uongozi huanzia, na hapa Zanzibar, skuli kama Memon Academy na Skuli ya Sekondari Benmbella zinachukua hatua kubwa kuhakikisha watoto wa kike wanapewa fursa ya kujifunza na kuongoza . Mpango wa Maendeleo wa Zanzibar 2050, unasimama kama nguzo muhimu ya kuendeleza vijana, hasa wasichana, kwa kuwaandaa kushika nafasi za uongozi wa siku zijazo. Mpango huu umejikita katika kukuza elimu na ustawi wa vijana,ambapo mbali na mpango huo, kuna na Sheria ya mtoto ya Zanzibar ya mwaka 2011, inayolenga kulinda haki za watoto, ikiwa ni pamoja na haki ya kupata elimu na fursa sawa za maendeleo ya uongozi. Kwa kupitia sheria hiyo tunashuhudia namna watoto wa kike wanavyopata fursa mbalimbali za kielimu, ikiwemo majukumu ya uongozi kwa nafasi za mawaziri wa darasa, viongozi wa michezo, na wakuu waklabu. Hiyo ni sehemu ya mchakato wakuwajengea uwe...