IMEANDIKWA NA ZUHURA JUMA, PEMBA MADAKTARI na wauguzi wa kituo cha Afya shehia ya Pandani wameshauriwa kuendelea kutoa huduma bora za kimatibabu ili jamii iwe na afya njema. Akizungumza mara baada ya kukabidhi taa katika kituo hicho, Mkaguzi wa shehia hiyo Inspekta wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Khalfan Ali Ussi alisema, licha ya changamoto wanazokumbana nazo lakini hawana budi kujitolea katika kazi zao. Alisema kuwa, ili jamii ipate maendeleo inahitaji watu wake wawe na afya njema kwa ajili ya kufanyakazi vizuri, hivyo ni vyema kwa madaktari kuendelea kutoa huduma bora kwa mgonjwa anaefika kituoni hapo kwa matibabu. "Kwa kweli madaktari wanafanya kazi kubwa, hivyo tuendelee kujitolea kwa moyo safi ili jamii ipate huduma bora na afya njema," alisema Mkaguzi huyo. Inspekta Khalfan aliwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa wafanyakazi wa kituo hicho kuhakikisha kinadumu kwa muda mrefu, kwani wao ndio walengwa w...