Skip to main content

Posts

Showing posts with the label KURA YA MAPEMA PEMBA SHUWARII

KURA YA MAPEMA PEMBA YAFANYIKA KWA AMANI

    NA WAANDISHI WETU, PEMBA ZOEZI la upigaji wa kura ya mapema, lililofanyika Zanzibar, kwa upande wa Pemba liliripotiwa kwenda kwa amani na utulivu, katika vituo kadhaa, vilivyopangwa kufanyikwa kwa zeozi hilo, leo. Waandishi wa habari walishuhudia vikosi vya ulinzi na usalama, vikizunguruka katika miji, mitaa na vitongoji mbali mbali, kisiwani humo. Wakati zoezi hilo likiendelea kwa watu maalum, wakiwemo walinzi wa amani na watendaji wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ‘ZEC’, wananchi katika miji ya Chake chake, Mkoani, Wete na Micheweni waliendelea na shuguli zao. Ilibainika kuwa, maandalizi ya zoezi hilo lilofanyika leo Oktoba 28 yalifanyika kuanzia jana Oktoba 27, kwa watendaji, wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa upigaji kura, kufunga vifaa kwa wakati. Akizungumza na waandishi wa habari Mratibu wa ‘ZEC’ Pemba Ali Said Ali, alisema hadi leo majira ya saa 6:55 mchana, hakujaripotiwa tukio lolote, lililozuia au kuashiria kuzuia zoezi hilo. Alisema, watendaji waliote...