Skip to main content

Posts

Showing posts from December 21, 2025

MATTAR AAHIDI KUZITATUA CHANGAMOTO ZA WATUMISHI HATUA KWA HATUA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ KATIBU Mkuu wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar Mattar Zahor Massoud, alisema changamoto zinazowakabili wafanyakazi wa wizara hiyo Pemba, zitatatuliwa hatua kwa hatua, ili wafanye kazi kwenye mazingira rafiki. Alisema, anayaelewa vyema mazingira wa tumishi walioko Pemba kwa kule kukaa kwa muda mrefu, akiwa kwenye nyadhifa tofauti, hivyo wizara itahakikisha inazitatua changamoto hizo. Katibu Mkuu huyo, aliyasema hayo hivi karibuni, wakati akijitambulisha kwake na kuzungumza na watumishi hao, na kusema anachoomba ni umoja na mshikamano miongoni mwao. Alieleza kuwa, baada ya kukutana na waratibu alielezwa changamoto kadhaa, ikiwemo suala la usafiri, kutoshirikishwa baadhi ya waratibu hasa uandaaji wa bajeti kuu, na kuahidi kuyafanyia kazi. Alisema, suala la usafiri wa vyombo vya maringi mawili, wizara yenyewe itanunua kwa aina ya vipaumbele vyake, ili kuhakikisha zile Idara zinazohitaji, zinafanikiwa. ‘’Kwa upande wa vyombo ...