NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ ILE dhamira ya Dk. Hussein Ali Mwinyi kuifungua Pemba kiuchumi kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa, sasa imefana. Kwani uzinduzi wa ujenzi wa uwanja huo na barabara ya Chake Chake- Mkoani, umezinduliwa rasmi Septemba25, mwaka huu, katika uwanja wa ndege uliopo Furaha Pemba. Ni furaha kubwa kwa wananchi wa kisiwa cha Pemba, kuona kwamba kitu ambacho wamekisubiri kwa muda mrefu, sasa kinakwenda kufungua uchumi wao. Maana serikali ya awamu ya nane, imedhamiria kufanya mageuzi ya makubwa katika sekta ya usafiri wa anga Zanzibar, kwa lengo la kuimarisha miundombinu ya utoaji wa huduma katika uwanja wa ndege wa Pemba. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla amezindua ujenzi huo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, jemedari wa uchumi. Makamu huyo anasema, ujenzi wa miradi hiyo ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025 ambapo malengo ya se...