Skip to main content

Posts

Showing posts from May 3, 2026

WIZARA YA MAENDELEO, WB, ZEEA WAKUTANA KIKAO KAZI ZANZIBAR

  NA MWANDISHI MAALUM, ZANZIBAR Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto leo Mai 07 imekaa kikao kazi na Benki ya Dunia kwa ajili ya kupitia mipango ya utekeleza ya Mradi wa Kukuza Usawa wa Kijinsia Tanzania- PAMOJA, unaotekelezwa na Wizara hiyo kwa Kushirikiana na Wakala wa Uwezeshaji KIuchumi (ZEEA). Akizungumza katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mradi wa PAMOJA Kinazini, Unguja. Mkurugenzi Idara ya Mipango, Sera na Utafiti, Wizara ya Maendeleo, Jinsia, Wazee na Watoto Ndugu Daima Mohammed Mkalimoto amesema kilao   hicho kimeleta tija kutokana na michango ya wadau iliyotolewa ili kuhakikisha utekelezaja wa Mradi unawanufaisha walengwa walikusudiwa wakiwemo wanawake na watoto. Ameeleza kwamba Mradi wa PAMOJA unalengo la kuwainua wanawake kiuchumi kupitia ZEEA, pia luwalinda na kuwahifadhi wahanga wa matukio hayo, hivyo   Benki ya Dunia wametoa maelekezo kwaajili ya kuleta ufani. Naye Mratibu wa Mradi wa PAMOJA Ndugu Aisha Abbas Seif amesema k...

SEKTA YA UMMA, BINAFSI, WAANDISHI WA HABARI WAPEWA ELIMU YA UWEKEZAJI

NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@ MRATIBU Idara ya mashirikiano ya sekta ya umma na binafsi  Said Salum Mohamed , amewataka waandishi wa habari kutumia vyema kalamu zao katika kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na mashirikiano baina ya serikali na sekta binafsi, katika uwekezaji wa masuala ya kijamii na kiuchumi ili wananchi kupata huduma bora zinazosimamiwa na sekta hiyo. Ameyasema hayo alipokuwa akizungimza na wadau wa habari katika mafunzo yakuwajengea uwezo kuhusiana na mashiashirikiano baina ya sekta za umma na binafsi yaliyofanyika ukumbi wa wakala uwezeshaji wananchi kiuchumi G omban i Chakechake Pemba. Alisema kuwa sekta za umma na  binafsi imekuwa na mipango ya kutoa  huduma bora za kijamii na kiuchumi ili wananchi wapate huduma hizo zenye kuleta maendeleo. "Hizi taarifa ziwafikie jamii na wawekezaji katika kutoa huduma bora za kijamii na kiuchumi kwa  kuyafikia malengo ya serikali ili wananchi wapate maendeleo,"alifafanua. Alifafanua kuwa uwekezaji wa umma na binafsi Pu...

MADEREVA WATAKAOPANDISHA NAULI KUKIONA, ABIRIA WAPEWA USHAURI HUU....

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WIZARA ya Ujenzi na Uchukuzi kisiwani Pemba, imewataka wananchi watakaodaiwa nauli mpya iwe kwenye dalala, bajaji au bodaboda kwa kisingizio cha kupanda bei ya mafuta, kuripoti katika vyombo vya sheria, kwani serikali haijatangaaza nauli mpya. Kauli hiyo, imetolewa na Ofisa Mdhamini wa wizara hiyo, Ibrahim Saleh Juma, wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi, kufuatia malalamiko ya wananchi, kulipishiwa nauli mpya hivi sasa. Alisema, serikali inaelewa vyema juu ya changamoto ya kupanda kwa nishati hiyo ya mafuta duniani, ingawa bado, tamko la kupandishwa nauli halijatolewa. Alieleza kuwa, serikali imekuwa na utaratibu wa kupokea mapendekezo ya upandishwaji wa nauli hiyo kutoka kwa madereva hao, na kisha kukaa pamoja, ili kuangalia uwezekono wa kupandisha ama laa. Ibrahimu alieleza kuwa, hadi sasa na tokea kupanda kwa nishati hiyo, serikali haijatangaaza nauli mpya, hivyo ni marufuku kwa dereva yeyote, kupandisha nauli hiyo. Alifafanua...

MAHUJAJI WATAKIWA KUACHA KUTUMIA SIMU WAKATI WA IBADA YA HIJJA-ABDULGHULAM

  IMEANDIKWA NA TATU MAKAME MAHUJAJI watarajiwa wameaswa kuacha kushughulikia simu wanapokuwa katika ibada ya Hijja, ili waweze kuitekeleza kwa utulivu, unyenyekevu na kupata radhi za Mwenyezi Mungu. Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Ali Abdulghulam Hussein, wakati akifunga mafunzo kwa Mahujaji watarajiwa iliyofanyika katika Ukumbi wa Shantimba, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja yaliandaliwa na Taasisi ya Khairat Hajj and Umra Travel. Alisema, ni muhimu kwa mahujaji kufuata miongozo wanayopewa na viongozi wa Hijja na kuepuka vitendo vinavyoweza kuharibu ibada hiyo, ikiwemo kutumia simu bila ulazima au kujihusisha na mambo yasiyo na tija. “Niwaase mahujaji watarajiwa msijishughulishe na mambo yasiyo na faida kama kuangalia michezo wakati wa ibada, hilo linaweza kuharibu utekelezaji wa nguzo ya tano ya Uislamu,” alisema Abdulghulam. Aidha, aliwataka kuwa wavumilivu katika kipindi chote cha ibada hiyo ili waweze kuitekeleza kikamilifu na...

UFUGAJI MATANGO BAHARI AJIRA YENYE GHARAMA NAFUU, USHIRIKA 'TUMUOMBE MOLA' KUVUNA 20/=MILIONI

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ ‘…….SEA Cucumbers’ ama matango bahari…... Na wingine huliita jongoo la pwani, ama kiazi bahari. Ni aina ya wanyama ama kiumbe, kinachoendesha maisha yake baharini. Kitango bahari, kina ngozi ngumu kiasi na mwili mrefu ambapo muonekano na maumbile yake ni sawa na kitango kinacholiwa nchi kavu. Kitango bahari, kinaendelea kufafanuliwa kwenye vitabu na mitandao kuwa, kina mwili mrefu wenye via vya uzazi, moja iliyo na matawi. Wanyama hawa, wanapatikana kwenye sakafu za bahari duniani kote, wakiwa wamegawanyika kwenye spishi zaidi ya 1,717. Ingawa nyingi zao, zinapatikana eneo la Asia-Pasifiki, ambapo kwa Zanzibar utafiti umeonesha zipo zaidi ya aina 35. Vitango bahari, huishi kwa kutambaa kwenye sakafu ya bahari, na kuweka hifadhi na kujisitiri kwenye matumbawe.   Maisha ya viumbve hawa, waliokua hawakuwa na thamani kwa zaidi ya karne moja Zanzibar, maisha yao yana mchango mkubwa katika ikolojia ya bahari, hasa katika kuisafisha. ...