NA AMRAT KOMBO, ZANZIBAR@@@@ SIKU zote baadhi ya watu wanaimani ya kuwa, mwanamke bado ni mama wa nyumbani pekee. Ambae anatakiwa kuchunga familia yake tu peke yake, lakini bila ya kufikiri kuwa mwanamke anaweza kufanya mambo makubwa ya kuwasaidia jamii na kuleta maendeleo katika nchi. Ushahidi wa hili, sasa usiangalia tena Marekani na kwengineko, njoo kwa Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania, alivokuwa jasiri na mchapa kazi, katika nafasi yake ya uwongozi. Hivyo inaonesha kuwa, mwanamke sio mdhaifu kama watu wanavoona, hebu tuangalie baadhi ya viongozi mwanamke wanavyowajibika katika nafasi zao. Fatma R as hid Juma ni diwani wa Chukwani Unguja, anasema kabla ya kushika nafasi hiyo, alikuwa mfanya biashara mjasiria mali mdogo, huku akiwa mwanancha wa chama cha mapinduzi CCM. Anasema katika mwaka 2020, alijishirikisha katika kugombea udiwani wakiwa na wagombea wenzake 11, wakiwa wanawake watatu na wanaume nane, na kubahatika kutokea mshindi kwenye kinyanganyiro hi