NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ SHILINGI milioni 107,190,000 zilizotarajiwa kukusanywa na Baraza la Manispaa Chake chake Pemba, kuanzia mwezi Novemba, 2023 hadi Januari mwaka huu, hazikupatikana, baada ya wajasiriamali kugoma kukitumia kituo chao cha Michakaini, kwa wakati. Imebainika kuwa, kituo hicho kipya kilichojengwa kwa ajili yao, kina milango 63 ya maduka, ambapo kila mmoja Baraza lilikusudia kuukodisha kwa shilingi 50,000 ili lijipatie shilingi milioni 3,150,000 kwa kila mwezi mmoja. Ingawa imebainika, baada ya wajasiriamali hao kukataa kuingia kituoni humo, Baraza hilo, kuanzia mwezi Novemba, 2023 hadi Januari mwaka huu, limeshapoteza shilingi milioni 85,050,000. Aidha mapato ya shilingi ya milioni 22,140,000 nayo hayakukusanywa na Baraza hilo kwa kipindi hicho, yaliokuwa yatokane na vizimba ‘ vikuta ’ 82, ambapo kila kimoja, kilitarajiwa kukukodishwa kwa shilingi 10,000 kwa wajasiriamali. Ikafahamika kuwa, vikuta hivyo kama vyengepata wajasiriamali, kw...