JUMA MUSSA, PEMBA. WAUMINI wa dini ya Kiislam wametakiwa kuishi kwa kuendana na malengo ya Qur- an ili kupata amani , maendeleo na salama hapa ulimwenguni na Akhera siku ya malipo. Afisa Mdhamini Tume ya Mipango Pemba Khamis Issa Mohamed aliyasema hayo Machi 3, 2023 kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa kusini Pemba Matar Zahor Massoud Ole Kianga katika ufunguzi wa Ijitimai ya 24 ya Kitaifa inayofanyika Kisiwani Pemba. Alisema bila kuwepo umoja, maadili mema na mshikamano hakuna maendeleo yatakayopatikana kutokana na umma kuwa na fadhaa jambo ambalo linatokana na kusahau maamrisho ya dini yao. “ Tusifichane ndugu zangu waislamu bila ya nchi kuwa na amani hakuwezi kupatikana maendeleo kwani kila mmoja atakuwa anapigania uhai wake na hatimae hata kufanya Ibada jambo ambalo tumeletewa hapa u limwenguni tutakuwa muda hatuna hivyo tutakuwa na makosa mbele ya Allah (S.W.T)”, alisema. Alifahamisha kuw...