NA NAFDA HINDI, ZANZIBAR JUMLA ya kazi 529 za waandishi wa habari zimewasilishwa TAMWA kwa ajili ya kuwania tuzo za umahiri za uandishi wa habari za takwimu za wanawake na uongozi. Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar, (TAMWA – ZNZ), Dkt. Mzuri Issa,amesema miongoni mwa kazi hizo ni pamoja na vipindi vya redio, televisheni, makala za magazeti na kutoka katika mitandao ya kijamii zilizoandikwa na kurushwa katika vyombo vya habari kuanzia mwezi Januari hadi Disemba 31, 2023. Dk Mzuri amesema lengo la tuzo hizo ni kuhimiza waandishi wa habari kutumia kalamu zao na vyombo vya habari kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa masuala ya wanawake katika uongozi na kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi mbalimbali za maamuzi. “Kazi hizo zinaonesha ni jinsi gani waandishi wamekuza mwamko wa kuandika habari za uongozi kwa wanawake ambapo zinashajihisha wanawake na vijana wakike kujiamini zaidi na kuwa na matuma...