NA HAJI NASSOR@@@@ WIZARA ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar, imesema katika Baraza la Wawakilishi linalotarajiwa kuanza wakati wowote, sheria mpya ya habari, itasomwa kwa mara ya kwanza. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa wizara hiyo Riziki Pembe Juma, jana Mei 2, 2026 hoteli ya Madinatul-Bahar iliyopo nje kidogo ya mji wa Unguja, kwenye hafla ya utoaji tuzo, kwa waandishi wa habari za takwimu, kuhusu wanawake na uongozi. Alisema, tayari kila kitu kimeshakaa sawa na kinachosubiriwa, ni kufika kwa siku ya kuanza kwa kikao cha Baraza hilo, na mswada huo kusomwa. Alisema, wizara imeshakamilisha taratibu zote, na sasa wadau wa sheria hiyo wakiwemo waandishi wa habari, wafuatilie Baraza la Wawakilishi lijalo. ‘’Najua mliowengi mnahamu ya kutaka kusikia, kuhusu nini wizara imefikia, juu ya sheria mpya ya habari, lakini niwaarifu kuwa, itapelekwa Barazani mwaka huu wa 2026/2027,’’alifafanua. Katika eneo ji...