KUCHELEWA KUHAMIA KWA WAJASIRIAMALI KITUO CHA MICHAKAINI, MANISPAA CHAKE CHAKE ILIKOSA 'BUNDA' LA MAPATO
NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@ MWENYEWE Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi kwenye hutuba yake ya ufunguzi wa Kituo cha wajasiriamali Chake chake, alielezea kufarajika. Mbele ya umati wa wajasiriamali na wananchi wa mkoa wa kusini Pemba, ameelezea kuwa, sasa atapa usingizi baada ya kumalizika kwa kituo hicho. ‘’Leo nimefarajika kuona sasa kituo hichi kipya na cha kisasa, nakifungua rasmi, sasa wajasiriamali wa mji wa Chake chake, waliokuwa wakihangaika huku na kule wamepata utulivu,’’akasisitiza. Eneo jingine Dk. Mwinyi wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo hicho, mwezi Oktoba 2023, akatoa rai kama sio maagizo kwa Baraza la Manispaa Chake chake. Moja, akaanza kusisitiza kwa watendaji, kuhakikisha usafi unafanyika kwa udhati, ili wananchi watakaofika hapo, wasishuhudie uchafu kuzagaa. Jingine akaelekeza, watendaji wa Manispaa na Halmashauri, kuhakikishe, hakuna hata mjasiriamali mmoja, anaepanga bidhaa zake nje ya soko hilo. ‘’Haiwezekani hata kidogo, kuwa w...