Skip to main content

Posts

Showing posts with the label MABADILIKO TABIA NCHI

MAENEO 148 YAATHIRIWA NA MABADILIKO TABIANCHI

  TAMWA ZNZ, Kitengo cha Habari SEREKALI ya Mapindizi ya Zanzibar imesema inaendelea na juhudi mbali mbali za kudhibiti athari za mabadiliko ya tabianchi ili kuhakikisha nchi inakua salama. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Harusi Said Suleiman alisema hayo alipokuwa akizungumza na wadau wa mazingira katika mkutano wa mabadiliko ya tabianchi katika ukumbi wa Shekhe Idrisa Abdul Wakili Kikwajuni Zanzibar. Alisema Zanzibar ni miongoni mwa nchi iliyoathirika na mabadiliko hayo katika nyanja mbali mbali ikiwemo za kiuchumi na kijamii. “Sehemu kubwa zilizoathirika katika maeneo hayo ni pamoja na kilimo, uvuvi, utalii na makaazi ya wananchi hali ambayo kwa namna moja au nyengine imesababisha kurudisha nyuma juhudi za wananchi na taifa kwa ujumla katika kukuza uchimi wa nchi,”alisema. Alisema mwaka 2012, Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais ilifanya utafiti ulionyesha kuwa hali ya hewa ya Zanzibar imeathirika kutokana na mabadiliko ya Tabianchi jambo lilosababisha ...