Skip to main content

Posts

Showing posts from March 30, 2025

WAZAZI WAMBAA WAAHIDI KUIUNGA MKONO KAMATI YA MAADILI

NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WAZAZI na walezi wa kijiji cha Kidutani, shehia ya Chumbageni Wambaa wilaya ya Mkoani Pemba, wameahidi kuiunga mkono kamati ya maadili na taaluma ya kijiji hicho, ili kuwadhibiti vijana kutojiingiza katika vigenge visivyo na tija, kwa maisha yao ya leo na kesho. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kijijini hapo, walisema mkakati ulioanzishwa na kamati ya muda, wa kuhakikisha wanawarejesha wanafunzi madrasaa, skuli na kuingia kwenye ibadaa ni wazo zuri, kwani manufaa yake ni makubwa. Walieleza kuwa, wazo hilo, ni vyema kila mzazi na mlezi, kukubaliana na mauelekeo wa kamati hiyo, kwani imekuja kusaidiana malezi ya pamoja,  na hasa yenye kufangamana na mwenendo , tabia na mafundisho ya dini ya kiislamu. Mmoja katia ya wazazi hao Shaibu Pandu Makame, alisema katika kufanikisha lengo hilo, huu ni wakati wa kuungan na kusahau tofauti zao walizonazo. Alieleza kuwa, suala la malezi katika karne hii limekua gumu, hasa baada ya kila mzazi, kutaka kumlea mtoto ...

WEMA YAPIGA MARUFUKU MICHANGO KUMUHUSISHA MWANAFUNZI

WAZAZI wa shehia ya Mgogoni Wilaya ya Wete Pemba wamelalamikia tabia ya walimu wa skuli ya Kinyasini kuwarudisha watoto wao skuli kwa ajili ya kuchukua pesa ya kufanyia mitihani, hali ambayo inarudisha nyuma maendeleo yao ya elimu. Walisema kuwa, hawajakataa kulipa fedha kwa ajili ya mitihani ya watoto wao kwani ni jambo zuri, ingawa kinachowauma ni vile kutolewa wakati masomo, hali ambayo inawakosesha vipindi vinavyoendelea skuli. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi wazazi hao walisema, wakati mwengine hawana pesa kutokana na hali ngumu ya maisha, hivyo huwapa pesa nusu kupeleka skuli ingawa hurejeshwa tena kwa vile hawajakamilisha, jambo ambalo linawauma sana. ā€˜ā€™Hatujakataa kulipia kwa sababu tunapenda wafanye mitihani, lakini linalotusikitisha ni hili la kuwatoa watoto skuli waje nyumbani kuchukua pesa, kwa sababu wanakosa masomo na jengine wanaweza kufanyiwa udhalilishaji njiani kwani ni masafa marefu,ā€™ā€™ walisema wazazi hao. Walisema kuwa, ni kilio kikubwa kwa skuli hiyo, kwan...

USHIRIKI WA WANAWAKE MAPAMBANO YA MABADILIKO YA TABIANCHI WAZAA MATUNDA@@@@

  NA KHAULAT SULEIMAN,PEMBA  KATIKA harakati za kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi, jitihada za akina mama zinazidi kwa kuandaa mbinu,  ambazo zitasaidia katika  kukabiliana na janga la mabadiko ya tabia ya nchi. Mabadiliko ya tabia ya nchi yanazidi kujitokeza siku hadi siku, kiasi ambacho husababishwa na  shughuli  za kibindamu, ikiwemo ukatwaji wa miti ya juu na ile ya pembezoni mwa bahari. Ambayo kisayansi yametajwa kuwa, husaidia kuzuiya upandaji wa maji juu ama kufika katika sehemu za makazi ya wanachi. Mabadiliko ya tabia ya nchi (climate change) ni  mwenendo wa hali ya hewa yakiwemo majira, wastani na vizio vya juu na chini kabisa vya joto, utokeaji  na mtawanyiko wa mawingu, mvua na theluji. Zipo athari kadhaa ambazo zinasababishwa na hali hiyo, ambayo huathiri jamii na nchi kwa ujumla. Moja wapo ni ongezeko la nyuzijoto, na kasi ya matukio mabaya mno ya hali ya hewa kuanzia kwa mawimbi na joto, ukame, mafuriko, dhuruba za msimu wa b...

KAMATI: 'MASHINDANI YA TANO YA QUR-AN WAMBAA YALIFANIKIWA'

NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ JUMUIYA ya tahafidhi qur-an kanda ya Wambaa na Chumbageni wilaya ya Mkoani, imewashukuru waumini wote na taasisi nyingine, kwa michango yao, iliyofanikisha mashindani yao ya tano ya tahafidh qur-an, yaliyofanyika hivi karibuni. Akizungumza kwenye kikao cha tathmini, kilichofanyika almdarsaatul- imaniya  Chumbageni, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ustadhi, Hassan Othman Khamis, alisema pamoja na kujipanga kwao, lakini michango ya wadau, ilisaidia kufanikisha shughuli hiyo. Alisema kuwa, umoja na mshikamano waliopewa na jamii ya Chumbageni na Wambaa, ni vyema ukawa endelevu kwani, wanamalengo ya kuendesha mashindani mingine makubwa, hapo mwakani. Alieleza kuwa, bila ya wanajamii kufanikisha michango yao, isingekuwa rahisi wao, kufikia malengo na kuendesha mashindani hayo ya tano kwa mwaka huu. ā€˜ā€™Kwa hakika michango ya fedha, vifaa na zawadi nyingine zilizotolewa na wanajamii, ilisaidia mno kunogesha mashindani yetu, na tunawapa shukran watu wote,ā€™ā€™alifafanua. Hat...