NA HAJI NASSOR, PEMBA::: KANUNI ya Utumushi wa Umma ya Zanzibar ya mwaka 2014, imeundwa na vifungu wastani wa 134. Kanuni hii, ni zao la sheria ya Utumishi wa Umma ya Zanzibar, ambayo nayo ilitungwa na Baraza la Wawakilishi, kwa lengo la kubainisha na kuweka wazi haki, wajibu wa watumushi wa umma. Kanuni hii, imekuja kufafanua na kuweka taarifa kwa upana zaidi kwa watumishi wa umma wa Zanzibar, ili kuongeza kasi, ari, hamasa na juhudi za kuwahudumia wananchi. Kanuni hii ya utumushi wa umma ambayo ilisainiwa Mei, 29 mwaka 2014 kazi iliyofanywa na aliyekuwa Waziri wa nchi ofisi ya rais, kazi, na utumishi wa umma Zanzibar Haroun Ali Suleiman. UTEKELEZAJI WA KANUNI HIYO Watumishi waliowengi wa umma Zanzibar, kwao kanuni hii imekuwa maarufu na kuitekeleza kwenye vifungu vichache ambavyo, pengine vinamsaidia mwajiri na sio mwajiriwa. Kwa mfano, wengi wa watumushi wa umma, wanaelewa kuwa kanuni hiyo inavifungu vya kuhimiza kufika kazini saa 1:30 na kuondoka saa 9:30 ka...