Na Salma Lusangi NAIBU waziri Wizara Maji, Nishati na Madini (WMNM) Zanzibar Shabaani Ali Othman ameagiza uongozi wa wizara hiyo kufikisha huduma ya maji safi na salama haraka katika Shehia ya Kizimbani Jimbo la Bububu, Wilaya Maghari ‘B’ ili kuwaondolea tatizo liliyopo. Akizungumza na wakaazi wa eneo hilo, alisema haiwezekani wananchi wakose maji kwa muda wa miezi minne hivyo aliitaka Uongozi wa Wizara yake kuhakikisha wakaazi wa shehia hiyo wanafungiwa mashine ya kusukumia maji katika kisima cha rasilihema ili wapate huduma hiyo. Alisema ikiwa changamoto kubwa ya maji katika eneo hilo inatokana na mashine ya kusukumia maji kuungua hivyo Wizara yake inajukumu la kufunga mashine nyengine ili wananchi wapate huduma hiyo. Alifahamisha kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kupitia wizara hiyo inatekeleza miradi mikubwa ya maji ili kuowandolea wananchi tatizo la maji safi na salama ikiwa ni ahadi ya Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la M...