NA MARYAM SALUM, PEMBA@@@@ WAANDISHI wa habari kisiwani Pemba, wametakiwa kutojihusisha na ishara zozote zinazopelekea uvunjifu wa amani, iwe ni kabla, wakati baada ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu. Wito huo ulitolewa August 28, 2025 na Mkurugenzi wa Baraza la Mji la Manispaa ya Chake Chake, Shida Kombo Hamad, kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Chake Chake, wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa wanahabari hao, juu ya kuripoti habari za uchaguzi, katika ukumbi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar ‘ZBC’ Pemba. Alisema kuwa vyombo vya habari ni taasisi muhimu kwa jamii nchini, vinavyotoa huduma ya kuhabarisha, ambayo ni haki ya msingi raia kama inavyotamkwa kwenye katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kifungu cha 18. Alieleza kuwa, dhima ya sekta ya habari ni kuelimisha na kuburudisha jamii, ambapo kwa upande wa utangazaji, sekta ya habari inahudumiwa na vyombo vya habari ambavyo ni redio, television na mit...