NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MKUU wa wilaya ya Wete Pemba, Abdalla Rashid Ali, amesema, uendelezaji wa kampeni ya msaada wa kisheria ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluh Hassan, ni chachu ya upatikanaji haki kwa wananchi wasiokuwa na uwezo. Mkuu huyo wa wilaya ya aliyasema leo Mei 31, 2025 ukumbi wa Jamhuri Wete, alipokuwa akifungua mafunzo ya wataalamu wa masuala ya sheria, kabla ya kwenda kutoa msaada wa kisheria wananchi wa wilaya ya Micheweni na Wete kwa siku tisa. Alisema, wazo la Mama Samia, ni jema ambalo pamoja na kuwasaidia wananchi kutambua haki zao za msingi, ni msingi wa kulinda na kuendelea amani iliyopo. Alieleza kuwa, iwapo wananchi watafundishwa namna ya kujua haki zao, itasaidia mno kuheshimiana katika mambo mbali mbali, samba mba na kukuza na kuendeleza msingi wa amani na utulivu. ‘’Kwanza niwapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na yule wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa, kuanzisha jambo hili...