NA MWANDISHI MAALUM, ZANZIBAR Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Wakili Dunford George Mpelumbe, amewahakikishia wanachi wa Zanzibar jinsi ya Tume hiyo ilivyojipanga vyema katika kupokea, kuchunguza na kutatua kwa wakati na usawa, malalamiko yote ya ukiukwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora yanayofikishwa katika ofisi za Tume hiyo zilizopo Zanzibar. Mhe. Mpelumbe ameyasema hayo leo tarehe 11 Novemba, 2026, alipozungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali katika Ofisi za Tume zilizopo Mombasa, Mkoa wa Mjini mMagharibi. Akitaja majukumu ya Tume kwa waandishi hao Mwenyekiti Mpelumbe aliwaeleza waandishi hao kwamba Tume mbali ya majukumu mengi iliyonayo, inatoa Elimu kwa Umma, kusimamia mikataba ya kimataifa kwa kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa mikataba yote ya kikanda na kimataifa inayohusu haki za binadamu ambayo Tanzania imeridhia. Pia alieleza namna ya Tume inavyoendelea na kushughulikia malalamiko ya wananchi ya...