NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ A FISA Mdhamini wizara ya Fedha na Mipango Pemba Abdul-wahab Said Abubakar, amezitaka asasi za kiraia Pemba, kuitumia ofisi yake, wakati wanapotaka kuandika miradi, ili kupata takwimu sahihi. Alisema, ili waweze kupata andiko lenye mashiko la mradi, hawanabudi kuwa karibu mno na ofisi hiyo, ili kupata takwimu sahihi, zinazotambuliwa na mamlaka husika. Afisa Mdhamini huyo aliyasema hayo, leo Novemba 24, 2024 ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Chake chake, alipokuwa akifungua mjadala kwa asasi za kiraia, juu ya changamoto za sekta zilizopo kisiwani Pemba zilizolalamikiwa kurudisha nyuma harakati za maendeleo kwa asasi na wananchi . Alisema, asasi za kiraia zimekuwa ndio mdomo wa changamoto zilizopo ndani ya jamii, hivyo wakiitumia ofisi yake, wanaweza kupata takwimu zinazoweza, kupata mashiko ya hoja zao. Alifahamisha kuwa, haiwezekani kwa asasi za kiraia, kukaa mbali na wizara ya Fedha, kwani imekuwa ndio eneo pekee lenye kukusanya kodi na tak...