Skip to main content

Posts

Showing posts from September 6, 2026

ZANZIBAR YAZINDUA MUONGOZO WA MAWASILIANO KATI YA MZAZI, MTOTO

  Na Mwandishi Wetu, Zanzibar@@@ SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar, kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), imezindua rasmi Muongozo wa Mawasiliano kati ya Mzazi na Mtoto kuhusu Haki ya Afya ya Uzazi (PCC Toolkit), unaolenga kuimarisha malezi, mawasiliano, ulinzi na ustawi wa watoto na vijana. Uzinduzi wa muongozo huo umefanyika jana katika Hoteli ya Verde na kuzinduliwa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Zawadi Amour Nassor, kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Anna Athanas Paul. Akizungumza katika hafla hiyo, Zawadi alisema wazazi na walezi wanapaswa kuvunja ukimya katika kujadili masuala ya afya ya uzazi na watoto wao kwa kutumia lugha sahihi, yenye heshima na inayozingatia umri wa mtoto. Alisema watoto na vijana wanahitaji kupata taarifa sahihi zinazolingana na umri wao ili kuwasaidia kuelewa mabadiliko wanayopitia, kutambua hatari, kujilinda dhidi ya ukatili na kufanya maamuzi sahihi kuhusu ...

KUELEKEA TAMASHA LA 31 LA UTAMADUNI WA MZANZIBARI MWAKA 2026 PEMBA, RESI ZA NGALAWA KUSHUHUDIWA

NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ UTAMADUNI, ni neno la lugha ya kiswahili, ambalo kwa lugha ya kiingereza ni ‘ culture ’, lenyewe likitokana na neneo la kilatini, lenye maana ‘ Cultura’ .   Mitandao ya kijamii, inaripoti kuwa, neneo hilo usuli wake ni neno ‘ colere’,  linalomaanisha "kulima, kustawisha.   Ikifafanua kuwa, neno hili linafafanuliwa kwa namna nyingi, ikiwemo tokea mwaka 1952, na Alfred Kroeber  na  Clyde Kluckhohn ,  walikusanya orodha ya vijelezi 164 vya neno hilo, katika kazi yao.   Miongoni mwa vijelezi hivyo ni ‘ c ulture:a’, critical, Review , ambapo lengo ni kuonesha mzizi wa neno, utamaduni kwa lugha ya Kiswahili, ama ‘ culture’ kwa lugha ya kiingereza. KWANINI MATAIFA YAWE NA UTAMADUNI? Inafahamika katika maandishi mbalimbali, kikiwemo kitabu cha ‘ukombozi wa kiutamaduni’ kuwa, utamaduni ni kielelezo cha uhai wa watu. Kwa mfano Tanzania pekee, imeundwa na mchanganyiko wa zaidi ya makabila 120, yenye mila, lugha ...

MRADI MKAKATI UJENZI WA MATANGI YA KUHIFADHIA MAJI PEMBA, NI NJIA YA KUJIKWAMUA NA KIPATO

  NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@ MAJI ni rasilimali muhimu kwa maisha ya viumbe wote wanaoishi. Kwa mujibu wa mitandao ya kijamii lita trillion 11 hadi 12.5 za maji, hutumika kwa siku duniani kote. Itambulike maendeleo yote duniani, hutegemea upatikanaji huduma muhimu za kijamii, ikiwemo maji safi na salama. Mitandao ya kijamii imeripoti sekta ya kilimo pekee inachukua karibu lita trillion 8.0 za maji kwa siku, ikifuatwa na ya viwanda inayokisiwa kutumia lita trillion 2.3, huku matumizi ya nyumbani yakikisiwa kuchukua lita trillion 1.2 duniani kote. Ndio maana, serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar huchukua juhudi za makusudi, kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama, kila siku. Miongoni mwa juhudi hizo ni utekelezaji mradi wa kimkakati, wa ujenzi wa matangi makubwa ya kuhifadhia maji, katika maeneo ya mikoa miwili ya kisiwa cha Pemba. Ofisa Mdhamini Ofisi ya Rais Pemba Shuweikha Abdallah Omar anasema, mbali na kusogeza huduma ya maji kwa wananchi, mradi ...