Skip to main content

Posts

Showing posts with the label WADAU WA HABARI

UPATIKANAJI SHERIA MPYA YA HABARI, WADAU WAHARAKISHA

  NA KHAULAT SULEIMAN, PEMBA@@@@ NI takriban miaka 20 sasa, shauku ya waandishi wa habari pamoja na watetezi wengine wa haki za binaadamu Zanzibar, kuona nchi yao inapata sheria rafiki za habari imekuwa ikitimizwa kwa maneno.  Viongozi wa ngazi mbalimbali serikalini, wamekuwa wakitoa ahadi lakini utekelezaji wake unasuasua. Tangu alipoingia madarakani, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amekuwa akionesha kutambua umuhimu wa sekta ya habari kuwa na sheria bora na rafiki. Akiwa amekalia kiti cha Ikulu baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, Dk. Mwinyi hakuchukua muda alitoa matamshi yenye mtazamo wa kupendelea waandishi wawe na uhuru zaidi wa kufanya kazi zao. Mara baada ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) kutoa ripoti ya utendajikazi wa vyombo vya habari, mwaka 2021/2022, ikieleza kuwa Zanzibar inahitaji sheria “mpya kabisa” za kusimamia sekta ya habari. Serikali ilijikuta inakumbushwa jukumu au wajibu wa kufanyia kazi suala hilo, kwa ku...