Skip to main content

Posts

Showing posts with the label MWANAMKE NA UONGOZI

CHUMU JUMA ABDALLAH: ANAYEINUA SAUTI YA WANAWAKE KATIKA UONGOZI

  Na AMRAT KOMBO , ZANZIBAR @@@ Kwa miaka mingi, siasa imekuwa ikitazamwa kama uwanja wa wanaume. Lakini kwa Chumu Juma Abdallah, mwanamke mwenye umri wa miaka 40, mtazamo huo unabadilika taratibu, Kutoka kuwa kijana aliyekuwa na shaka ya uwezo wake.  leo amekuwa kiongozi anayetazamwa kwa heshima, akigombea Uwakilishi wa Viti Maalum na nafasi ya Makamu Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Alliance for African Federal Party (AAFP) kwa upande wa Zanzibar. “Nilianza nikiwa ninaogopa, nikiamini siwezi, lakini viongozi wangu walinipa moyo. Waliniambia ninaweza, nami nikaamua kuthibitisha,” Amesema Chumu. Safari ya Chumu kielimu ilianza mwaka 1990 katika Skuli ya Msingi Hurumzi, kisha akaendelea na Skuli ya Sekondari Hamamni mwaka 2000. Mwaka 2002, alijiunga na Chuo cha Muslimu Mazizini, hatua aliyosema ilimsaidia kujijenga katika maadili na kujiamini. Akiwa mtoto wa nne kati ya watoto nane wa Mzee Abdallah, Chumu anakumbuka jinsi wazazi wake walivyokuwa na mashaka kuhusu azma yake ya kuin...