Skip to main content

Posts

Showing posts from October 22, 2017

Wanaojipamba wakienda kuokota mpeta wana ajenda gani ya siri? Pemba

IJAPOKUWA kuanzia serikali za wilaya, mkoa hadi taifa zimeshapiga marufuku kwa wanawake, watoto na watu wengine kuacha kabisa kuokotoa karafuu zinazoanguka “ mpeta ” lakini bado wengine wanaendelea kupuuzia agizo hilo . Wapo wanaoendelea kuokota mpeta wakiwa na watoto wao, ingawa sababu za kuokota mpeta wenyewe huwa wanazo na pengine ukizisikiliza zinaweza kuingia akilini. Maana wengine husema kama ni vitendo vya udhalilishaji, basi vipo hata kabla ya ujio wa zao hili la karafuu, na ndio maana wanadai kuwa anaetaka kudhalilishwa hata kama hakuna karafuu. Lakini kubwa na lililonileta mbele yenu leo hii na kuutumia ukurasa huu, ni kuwauliza hawa wanaokwenda kuokota mpeta wakiwa wamejipamba wana ajenda gani huko? Maana utashangaa wakati ukipishana nao au kama utabahatika kupanda gari moja nao, jinsi walivyojipura kama sio kujiremba. Kiutamaduni kila mmoja anaekwenda kazini hukoga na kujipura jinsi awezavyo, ingawa kila ina mazingira yake, lakini sio kuokota mpeta na kujipambana mbon...

‘JUMWAMPE’ YAGUNDUA HAYA KWA WAKULIMA

NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMATI ya Ushawishi na Utetezi kutoka Jumuia ya mtandao wa wakulima wa matunda na mboga mboga Kisiwani Pemba JUMWAMPE, imesema imegundua changamoto kadhaa zinawazowakabili wakulima wao, ikiwa ni pamoja na kukosa elimu ya matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo. Kamati hiyo, ilipita kwa wakulima zaidi ya 100 kisiwani humo, na baada ya kuwajazisha dodoso maalum, waligundua kuwa wakulima hao, hawana elimu ya matumizi ya dawa za mimea, hali inayotishia usalama wao na walaji. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mjini Chakechake mara baada ya kumalizika kwa safari ya kuwatembelea wakulima, Katibu wa Jumuia Mtandao huo Hamad Ali Mussa, alisema wapo waliowagundua kutumia dawa ya kuulia kunguni kwa kutumia kwenye mazao. Alisema jengine waliloligua wakati wakiwa na wakulima hao, ni kutokuwa na kipimo sahihi cha kunyunyizia dawa hizo, kwenye mboga mboga zao, ambpo hupelekea muda mfupi baada ya kutia dawa kuvunwa na kuuzwa sokoni. Katibu huyo alieleza ku...

LIGI DARAJA LA KWANZA TAIFA - PEMBA

Timu ya Mkoroshoni jana imefanikiwa kujichukuliwa point tatu muhimu baada ya kuifunga timu ya Tekeleza ya Mavungwa kwa mabao mawili kwa moja Magoli ya Mkoroshoni yamefungwa na Haroub Sheha kwa njia ya penalty katika dakika ya 60 na Farid Khamis dakika ya 71, na goli la Tekeleza limefungwa na Khalfan Omar dakika ya 33

Kigwangallah: Sihongeki na Wala Sipo Tayari Kuuza Utu Wangu Kisa Umasikini na Tamaa

Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla amesema ataendelea kuwepo ndani ya wizara hiyo kama kilichowafanya watangulizi wake kuondoka ni masilahi binafsi, kwa kuwa hahongeki, hashawishiki na aliyemteua analifahamu hilo. Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla amesema ataendelea kuwepo ndani ya wizara hiyo kama kilichowafanya watangulizi wake kuondoka ni masilahi binafsi, kwa kuwa hahongeki, hashawishiki na aliyemteua analifahamu hilo.  “Sitakuwa tayari kupoteza heshima yangu, aliyeniteua anajua kuwa mimi ni muarobaini wa hayo yote, hata nilipoteuliwa walianza kunidhihaki kupitia mitandao ya kijamii kuwa ninakwenda kuharibikiwa huko, eti kwa sababu mawaziri hawadumu, haipo hiyo,” alisema Dk Kigwangalla jana Jumapili Oktoba 22,2017 mjini Dodoma. Alisema hayo akijibu kauli ya Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro aliyemtahadharisha kuwa mawaziri wamekuwa hawadumu ndani ya wizara hiyo kutokana na kununulika na wadau kwa kuwa kuna ushawishi mwingi. Ha...