Skip to main content

Posts

Showing posts with the label ZSSF NA WADAU PEMBA

WADAU UANDAAJI MALIPO 'ZSSF' PEMBA TUMIENI MIFUMO KURAHISISHA TAARIFA

  NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@ AFISA Mdhamini Wizara ya Fedha na Mipango Pemba, Abdulwahab Said Abuu-bakar aliwataka wadau wanaohusika na uandaaji wa malipo ya michango katika mifumo ya Mfuko wa hifadhi ya jamii (ZSSF) kutumia mifumo hiyo kwa usahihi ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa wanachama wake. Aliyasema hayo April 15, 2025 katika mkutano wa kuwajengea uwezo wadau hao uliofanyika katika ukumbi wa (ZSSF) Tibirinzi Chake Chake Pemba. Alisema kumekua na malalamiko ya ucheleweshwaji wa upatikanaji wa mafao ya ustaafu kutoka kwa wanachama, yanayosababishwa na taasisi kushindwa kuweka kumbukumbu vizuri, katika mifumo hiyo. Hivyo alisema ni vyema kwakila taasisi kuhakikisha inatimiza majukumu yake vizuri ili kupunguza malalamiko hayo kwa wastaafu wa serikali na taasisi binafsi. "Ni vyema  taasisi zihakikishe  zinatimiza majukumu yake vizuri ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wastaafu wa serikali na taasisi binafsi" alisema. Alieleza kua  serikali imeandaa utara...