NA HAJI NASSOR, PEMBA:: KUMBE masuala ya haki za binadamu, yalianza kuingizwa katika mikataba mbalimbali ya kitaifa mwaka 1950. Na kwenye Azimio la kulinda Haki za Binadamu Ulimwenguni lilifikiwa mwaka 1984 na Afrika mwaka 1981. Baada ya hapo, mikataba ya kikanda ilipitishwa, kwa dhamira ya kutoa ulinzi wa haki za kiraia na kisiasa, haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni, kwa ufanisi zaidi. Maazimio mbali mbali, yaligusia juu ya suala la uhuru wa maoni na kujieleza, likiwemo azimio la ‘UDHR, katiba ya Zanzibar ya mwaka kifungu cha 18 (1) na (2) kama nayo imeeleza: “Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta kupokea na kutoa habari na dhana kupitia chombo chochote, bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati” Hata kifungu cha (2) ‘’kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbali mbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kw...