NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@ SIFUNI Ali Haji ni Katibu Mkuu na ni kiongozi wa mwanzo, anaefanya kazi na mtandao wa asasi za kiraia katika kisiwa cha Pemba, akiwa wa kwanza mwanamke. Anasema mtandao huo unaojulikana kwa jina la PACSO, ni Umoja wa Jumuiya zisizo za kiserikali uliyoanzishwa mwaka 2005. Katika safari ya uongozi wake, anaendelea kuzisimamia jumuiya na wanachama waliokuwa Pemba ikiwemo Pegao, Juwauza, na Tamwa. Sifuni anaendelea kuvunja vikwazo vyake, katika Jumuiya hiyo kwa zaidi ya miaka sita, akilenga macho yake katika mkoa wa kusini na kaskazini mwa mji wa Pemba. Kutokana na juhudi zake na moyo wa kujituma, amekuwa akilenga uwezo wa kusimamia maendeleo endelevu kwa jamii ya kisiwa hicho. ‘’Nafasi hii haikuja tu, baada ya juhudi zangu nilizokuwa nikizifanya katika uwanachama wangu, ndipo nilipopigiwa kura kwa asilimia zote kushika nafasi ya katibu, anafafanua. Zaidi ya mwaka mmoja taasisi hiyo, haikuwa na mafaniko yoyote baada ya kusimamiwa na wanaume, ndip...