NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ NAIBU Katibu mkuu wizara ya Nchi, Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Omar Haji Gora amewakumbusha watunza kumbu kumbu wa tasisi za serikali, kuwa, roho ya wizara ya ni sehemu za masjali. Naibu Katibu mkuu huyo, aliyasema hayo, kwa nyakati tofauti wakati akiyafungua mafunzo ya siku mbili, kwa makatibu muhutasi na watunza kumbu kumbu za serikali, kisiwani Pemba. Akizungumza na watunza kumbu kumbu hao, kwenye mafunzo yaliyofanyika ukumbi wa wizara ya Fedh Gombani, alisema masjali ndio eneo nyeti pekee, katika kila wizara. Alieleza kuwa, ofisi hiyo ndiyo inayotegemewa na wafanyakazi wote, kwa kuhifadhi kumbu kumbu zao mbali mbali, kama vile barua za ajira. Naibu Katibu mkuu huyo, alisema masjali sio sehemu ya kuwekwa ovyo ovyo, na inatakiwa kuangaliwa kwa macho zaidi ya mawili, kwani ni eneo la kutunzia haki za wafanyakazi. ‘’Msipokuwa makini kwenye masjali, mnaweza kumsababishia mfanyakazi, ugonjwa, maradh...