Skip to main content

Posts

Showing posts from July 19, 2026

LUGHA CHAFU ZA WAZAZI KWA WATOTO, ZINAVYOWARUGIA MIFUMO YAO YA MAISHA

  NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@ MALEZI bora na makuzi ya mtoto, ni jambo   muhimu kwa maendeleo yake,kimwili na kiakili. Hili linajumuisha huduma zote muhimu anazostahili kupewa mtoto, kuanzia miaka 0 hadi 8, ili kumuwezesha kukuwa na kufikia utimilifu wake. Ikiwa ni kimwili, kiakili, kijamii, kihisia na kimaadili, ilikushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa na kuyamudu mazingirayake. Mara nyingi ni rahisi kupata haya yote, kutoka kwa wazazi au walezi,lakini wengi wao husahau kwamba matumizi ya lugha nzuri kwa watoto,inamchango mkubwa katika ustawi wao. Na zipo sheria zinazopinga ukatili wa aina zote dhidi ya watoto, kwamsingi kwamba malezi bora kwa mtoto, ndio msingi imara kwa makuzi yake. Mfano, Mkataba wa kimataifa wa haki za watoto duniani ( Conventionoftherightsofthechildren ) wa mwaka 1989, ambao umeanza kutumikarasmi mwaka 1990. Ibara yake ya 19 inasisitiza, kuwa‘ nchi wanachama kuhakikishawanakuwa na sheria nzuri zitakazo mlinda mtoto juu ya aina zote zau...

TAMU, CHUNGU USAFIRI WA UMMA KWA WATU WENYE ULEMAVU, HADI VIGARI VYAO WALIPISHWA KAMA MZIGO

  NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@ UDHALILISHAJI katika vyombo vya usafiri ni pamoja na ukatili wa kijinsia, inayoashiria uvunjifu wa haki za binaadamu. Kwa wenzetu wenye ulemavu, wao wamekuwa nambari moja kudhalilishwa, wakati wanapokwenda ama kurudi kwenye mipango yao ya maisha. Hali hiyo hujumuisha kuguswa mwili bila ridhaa, matusi, kauli za kubaguliwa au kulazimishwa kukaa katika mazingira yanayoshusha heshima na utu wao. Mkurugenzi wa Jumuiya ya watu wenye ulemavu Juma Kombo Hija Pemba anasema, vyombo vya usafiri havipo rafiki kwao.   Anasema ukiangalia Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimeridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa, inayolenga kuweka mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu, pamoja kusimamia haki zao. Katika kuweka mazingira mazuri ni pamoja kusimamia haki zao na ujumuishwaji katika vyombo vya usafiri, hususana watu wenye ulemavu wa viungo. Anasema yapo matukio matatu yaliyoripotiwa kwa mwezi Juni na Jualai mwaka huu, katika jumuiya hiyo amabapo mt...

NADYA JUMA : KIJANA ANAEANZA POLE POLE KUUSAKA UONGOZI, ALIPOANZIA PATAMU

  NA ZUHURA JABIR, ZANZIBAR@@@@ "Uongozi hauanzi unapopewa cheo; huanza pale unapokuwa tayari kuwahudumia wengine,’’ kauli hii inaelezea kwa ukamilifu safari ya Nadya Juma Idrissa, kijana ambaye ameonyesha kuwa uongozi wa kweli hujengwa kwa kujituma, nidhamu na huduma kwa jamii.   Katika kipindi ambacho vijana wengi bado husita kushiriki katika masuala ya uongozi, Nadya, aliamua kuchukua hatua mapema.   Alianza kama mwanachama wa kawaida wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), lakini leo ni Katibu wa Hamasa wa Tawi la ‘UVCCM’ katika Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU). Safari yake ni ushahidi kwamba mafanikio hayaji kwa bahati, bali hujengwa hatua kwa hatua.   MWANZO WA SAFARI YA UONGOZI Nadya anasimulia kuwa, safari yake ilianza akiwa bado mwanafunzi, alipokuwa akishiriki kwa hiari, katika shughuli mbalimbali za CCM kwenye tawi la eneo analoishi. Hakuwa na cheo wala mamlaka, lakini alijitokeza kila mara, kushiriki shughuli za chama, mikutano na kazi za kujitolea. ...

WAZIRI ANNA PAUL AZIFARIJI FAMILIA ZILIZOPOTEZA WATOTO MBUZINI, ATOA WITO WA KUIMARISHA ULINZI WA WATOTO

  WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Anna Athanas Paul, leo amewatembelea na kuwapa mkono wa pole familia zilizopoteza watoto watatu kufuatia tukio la kusikitisha la kuzama kwenye bwawa la maji katika eneo la Mbuzini, Wilaya ya Magharibi A, Unguja. Akizungumza wakati wa ziara hiyo ya kuwafariji wafiwa, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za vifo vya watoto hao na inaungana na familia zilizopoteza Watoto wao wapendwa pamoja na wananchi wote wa Mbuzini katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. Amesema tukio hilo ni pigo kubwa kwa Taifa na limetoa funzo kwa jamii kuhusu wajibu wa pamoja wa kulinda usalama wa Watoto ni wajibu wa kila mtu katika jamii na sio wazazipekee. “ Tukio hili ni pigo kubwa kwa taifa na linatoa funzo kwa jamii, kuhusu wajibu wa kumlinda mtoto si la Serikali pekee bali kila mmoja wetu anawajibu wa kumlinda mtoto kwa kuzuia kila tukio hatarishi” Amesema Waziri Anna. Aidha Waziri ametoa wit...