IMEANDIKWA NA REHEMA MOHAMED PEMBA@@@@ JAMII inashauriwa kuwa karibu na watoto wenye ulemavu, ili kuwapatia haki zao za msingi ikiwemo elimu.zuh Hayo yalizungumzwa na sheha wa shehia ya Chambani wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko kijijini kwao. Alisema kuwa, watoto wenye ulemavu wanahitaji zaidi uangalizi wa mama na baba na sio kumuachia mzazi mmoja peke yake au kumtelekeza kwa bibi. Alisema, katika jamii kuna baadhi ya watu mara baada ya kupata mtoto ambae ana ulemavu, huamua kumtenga na kumuachia katika uangalizi wa mzazi mmoja hususani mama ili kuweza kukaa nae na baadhi ya wakati kushindwa kuwapatia hata huduma. Alieleza kuwa, si jambo la busara kabisa kwa watoto wenye ulemavu kuwaweka nyumbani bila ya kuwapatia elimu, kwani nao wanayo haki ya kupata elimu bora, kupatiwa matibabu pamoja na mahitaji mengine kama watoto wengine. Vile vile alisema kuwa, ni vyema jamii iondoshe itikadi mbaya ya kuwa mtoto mwenye ulemavu hawezi kufanya chochot...