NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ IDARA ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar, imemkabidhi ripoti ya awali, ya kampeni ya msaada wakisheria ya Mama Samia, mara baada ya kumalizika kwa kambi ya siku 10 ndani ya mkoa huo. Kabla ya kukabidhi kwa ripoti hiyo, Mkuu wa Idara hiyo Pemba Bakari Omar Ali, alipongeza ushirikiano alioupata kutoka kwa maafisa wa taasisi mbali mbali za serikali, wakati wote wa kampeni hiyo. Alisema, katika kampeni hiyo, waliwatumia maafisa wa kamisheni ya wakfu, ardhi, mawakili wa serikali, makadhi, maafisa ustawi, matukio ya kijamii pamoja na waandishi wa habari. Alieleza kuwa, maafisa hao walisaidia kwa kiasi kikubwa, kupokea malalamiko na kuyapatia ufumbuzi papo hapo na mingine kuziandikia barua taasisi husika. Alifahamisha kuwa, kampeni hiyo ambayo ilikuwa katika mifumo miwili, moja ni kuwafuata wanafunzi wa skuli, vyuo vya elimu ya juu pamoja na mikutano ya jamii. ‘’Tulijigawa timu mbili, moja wilaya ya Micheweni na nyingine Wete, ambapo maafisa k...