Skip to main content

Posts

Showing posts from March 22, 2026

CFP YAANZA KUMALIZA KIU YA UKOSEFU WA MAJI KWA WAKULIMA KILIMO MSITU PEMBA, FATMA BAKAR AANZA KUUAGA UMASKINI

NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@ ….nilianza na shamba moja la ekari moja, na sasa nimeongeza mawaili yenye ukubwa na nusu nusu eka kila moja, ndio maneno ya mkulima kilimo msitu Fatma Bakari wa Chato. Chato hiyo, sio ile ya Mkoani Dodoma Tanzania bara, hapana ipo kijiji cha Gombeume, shehia ya Mchanga mdogo wilaya ya Wete Pemba. Hapo ndio anapoishi mkulima huyo, ambae kwa sasa anajiita mtaalamu wa kilimo msitu, ama kilimo mchanganyiko wa miti ya biashara na chakula. ALIANZAJE KILIMO MSITU Alianza kuwataja Jumuiya ya Uhifadhi yaw a Misutu Pemba ‘CFP’ na Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA-Zanzibar, kwamba ndio waliomzua yeye na sasa kuwa mkulima mtaalam wa kilimo msitu. Alijifunza nini maana ya kilimo hicho, kinalimwaje na faida zake za muda mfupi na mrefu, katika maisha ya kila siku. Baada ya mafunzo, huku na muume, akiwa ameshafariki, ndipo mwaka 2024 mwezi wa August, alipoanza kilimo hicho ndani ya shamba la urithi la aliyekuwa muume wake. Hapo akiwa na utaalamu, ...

UZINDUZI MBIO ZA MWENGE WA UHURU KITAIFA 2026, NI ZAMU YA MKOA WA KUSINI PEMBA

NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ CHIMBO la mwenge wa Uhuru, ni nia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kuweka mwenge juu ya kilele cha mlima Kilimanjaro. Lengo ni kuleta matumaini pale pasipo na matumaini, upendo pale penye chuki na heshima pale palipojaa dharau. Ambapo nia hiyo, aliitoa kwa mara ya kwanza mwaka 1959 huko New York, alipohutubia Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa. Kwa wakatu huo, alimteua Luteni Alexander Gwebe Nyirenda kutekeleza azma hiyo iliyoitwa “Operesheni Mwangaza”, ambapo yeye na wenzake, walianza maandalizi mwezi Novemba 1961. Kabla ya Tanganyika kupata uhuru, ambapo hatimaye usiku wa mkesha wa sherehe za uhuru tarehe 9 Desemba 1961, Luteni Nyirenda na wenzake, waliwasha na kusimika mwenge wa uhuru na Bendera ya Tanganyika kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro. Hiyo ilikuwa kama ishara ya kuwa huru, kwa kupandisha mwenge kileleni ilikuwa kwanza, ni kuonesha kazi ngumu iliyoko mbele ya kulijenga taifa changa la Tanganyika. Pili, ilikuwa ni ku...