NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI wa shehia ya Wingwi Mjananza wilaya ya Wete Pemba, wamekishauri Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ kuhamishia ofisi kwenye shehia yao, ili kila wanapokuwa na changamoto zao za kisheria wawe karibu nao. Walisema, huduma walizopewa za ushauri wa kisheria bila ya malipo, zimewavutia na kuona ipo haja kwa sasa, kwa kituo hicho kujenga ofisi shehiani mwao. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi leo April 18, 2025 mara baada ya kufungwa kwa kambi ya siku tatu ya utoaji elimu, ushauri na msaada wa kisheria, walisema wanatamani ZLSC ijenga ofisini eneo la Mjananza. Walisema kuwa, wengi wao walikuwa hawana uwelewa wa utaratibu wa kufuatilia nyaraka kama za vyeti vya ndoa, talaka, vyeti vya kuzaliwa, vitambulisho jambao ambalo wamelipata ndani ya kambi hiyo. Mwananchi Salim Hamad Faki, alishauri kuwa, ni vyema kwa ZLSC ikawa na ofisini ngazi ya shehia, ili kupunguzia dhiki za wananchi kuwafuata mjini wanasheria, wanapokuwa na changamoto za...