HABIBA ZARALI, PEMBA
TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina
katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa
mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na
jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi.
Mtoto huyo
ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na
kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji
uliodumu kwa muda wa saa tatu na kuokolewa
maisha yake.
Akizungumza mara baada ya operesheni
huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo
kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika
hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana
kutokana na hali ya umaskini wa familia ya mtoto huyo.
Alisema timu
ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu kwa wananchi kisiwani humo, ili kuwaondolea gharama ya kutafuta matibabu
nje ya nchi hasa ukizingatia wengi wao ni wanyonge.
“Operesheni
hii tulidumu nayo kwa masaa matatu kwani ilikuwa ni kubwa na ngumu kiasi
ambacho asingefanyiwa ingeweza kuharibu mfumo wake wa mkojo, lakini tumeweza
kufanikiwa.”alisema.
Alifahamisha
kuwa katika kufanikisha upasuaji huo walikuwa na mawasiliano ya karibu na
mtaalamu wa magonjwa ya mfumo wa mkojo aliyeko kisiwa cha Unguja Dk Guo ambae aliweza
kutowa maelekezo mwanzo hadi mwisho wa upasuaji huo.
Hata hivyo
aliahidi kwa timu ya madaktari hao kueendelea
kutowa huduma za matibabu kwa wananchi
kisiwani humo, ili kuwaondolea gharama
ya kutafuta matibabu nje ya nchi.
Kwa upande wake Dk Shi wa idara ya uzazi na uzazi hospitalini hapo
alisema waliweza kushirikiana vyema baada ya kupata taarifa hiyo kutoka kwa Dk. Chang wa Idara ya Upasuaji hospitalini
hapo
“tukashirikiana timu nzima kufanya
kila jitihada kumuokowa mgonjwa ingawa kila mtu alikuwa amerowa na kuchoka
kimwili na kiakili, na tulihisi kuwa tumefanya jambo la busara”alisema .
Nae kaimu mganga mkuu hospitali ya Abdalla mzee Said Ismail Ali,
aliipongeza timu hiyo ya 32 ya madaktari wa kichina kwa uzalendo wao wa
kusaidia jamii kisiwani hapa.
Akitowa
shukrani baba mzazi wa mtoto huyo Omar Ali alisema ni jambo jema lenye kuleta
faraja walilofanya madaktari wa kichina kwa kumfanyia matibabu mtoto wake ambae
alihitajika kusafirishwa nje ya nchi jambo ambalo ni haikuwezekana kutokana na
ugumu wa hali yake ya maisha.
Upasuaji
huo ni wa mwanzo kwa ukubwa ambao wameufanya madaktari wa timu ya 32 katika
hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani tokea pale walipofika mwanzoni mwa mwezi wa
Oktoba.
Mwisho.
Comments
Post a Comment