HABIBA ZARALI, PEMBA KITUO cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC, kimeitaka jamii kisiwani Pemba, kuendelea kutoa elimu ya sheria inayohusiana na utatuzi wa migogoro na ujenzi wa amani, wanayoipata kupitia kituo hicho, ili kuifanya jamii kuishi kwa usalama na kupata haki zao. Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa kituo hicho tawi la Pemba, Safia Saleh Sultan, katika mkutano wa kutoa elimu ya utatuzi wa migogoro, uliowashirikisha viongozi wa dini, kisiasa na wahamasishaji jamii kutoka shehia za Njuguni na Mihogoni Wilaya ya Micheweni. Alisema elimu inayotolewa kituoni hapo, kupitia makundi mbalimbali ya jamii kisiwani humo, ni miongoni mwa njia wanazozifanya za kuhakikisha wanawajengea wananchi uwezo wa kisheria ili waweze kutatuwa migogoro kwa njia ya amani. Alieleza kuwa, katika jamii kuna migogoro mingi ikiwemo ya kesi za madai kama vile ya ardhi, ndoa, matunzo ya watoto, madeni, hivyo ni vyema wakavitumia vikao vya familia, kuyamaliza. ‘’Kesi kama hizi mnapokimbilia...