Skip to main content

Posts

Showing posts with the label LSF

LSF, IDARA YA KATIBA NA MSAADA WA KISHERIA ZANZIBAR UDUGU WAO KUENDELEA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ AFISA Miradi Mwandamizi kutoka shirika la ‘LSF’ ofisi ya Zanzibar Bakar Hamad, alisema wastani wa shilingi bilioni 5.1 zinaendelea kutumika kuanzia mwaka 2023, kwa ajili ya kusaidia msaada wa kisheria, kwa Tanzania bara na Zanzibar. Alisema, kati ya fedha hizo, asilimia 30 zimeekezwa Unguja na Pemba, kupitia wasaidizi wa sheria na Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar. Hayo aliyasema hivi karibuni, wakati akitoa salamu za shirika hilo, kwenye siku ya kwanza ya jukwaa la nne la msaada wa kisheria Zanzibar, lililofanyika mjini Unguja. Alisema, fedha hizo ambazo hutolewa kama ruzuku, zinalengo la kuimarisha msaada wa kisheria, ili haki iweze kupatikana kwa wnanachi, hasa wanyonge na wale wa makundi ya pembezoni. Alieleza kuwa,  kiasi hicho cha fedha kimeekezwa zaidi katika utoaji wa huduma za msaada wa kisheria,  elimu ya kisheria kwa jamii pamoja na kuwawezesha wanawake kwenye eneo la kiuchumi. ‘’Kupitia uwekezaji wa fedha hizo, LSF imes...