NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, imewatahadharisha wazazi, walezi na vijana wanaosubiri ajira za uwalimu, kuwa makini kwani, kwani matapeli wanaweza kuingilia kati zoezi hilo. Wizara hiyo imesema, matapeli wanaweza kuwahadaa wazazi, walezi au wataka ajaira hizo, na kuanza kuwapa maelekezo mingine yasiokuwa au yanayofafana na ya wizara, ili kuwatoleshea fedha. Akizungumza na waandishi wa habari Pemba, Katibu Mkuu wa wizara hiyo Khamis Abdalla Said, alisema ni kweli, katika mwaka huu wa fedha, wizra inaompango wa kuajiri waalimu, lakini nao matapeli wanaweza kutumia fursa hiyo. Alieleza kuwa, ndio maana wizara imeona iwatahadharishe wazazi na vijana wenyewe mapema, ili zoezi litakapoanza lisije kuwaathiri wananchi. Katibu mkuu huyo alieleza kuwa, maana wakati huo wa zoezi likiwa katika mchakato, wapo wanaoonekana kulalamikiwa, baada ya kupigiwa simu wakiahidiwa kusaidiwa kupata ajira hizo. ‘’Wizara ya Elim una Mafunzo ya Amali, i...