NA ZUHURA JUMA, PEMBA: ZAIDI ya watu 300 kutoka nchi mbali mbali ikiwemo Marekani, wanatarajiwa kushiriki katika Kongamano la sita la Kiswahili la kimataifa, litakalofanyika Disemba 17 na 18 katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete mkoa wa Kaskazini Pemba. Akizungumza na waandishi wa habari Afisa Mdhamini Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana, Utamaduni na Michezo Pemba, Mfamau Lali Mafamau alisema kuwa, maandalizi ya Kongamano hilo yameshafikia asilimia 90. Alisema kuwa, ni faraja kwa kisiwa cha Pemba, kufanyika Kongamano hilo, kwani wananchi walio wengi, watanufaika kwa namna mbali mbali kutokana na wageni watakaoingia pamoja sambamba na kujifunza mambo mbali mbali ya Kiswahili na utamaduni. ‘’Kwa kweli tunaona fahari Kongamano hili kufanyika kisiwani hapa, wageni wengi wataingia na kushiriki, hivyo wananchi watanufaika kwa namna moja ama nyengine’’, alisema Mdhamini huyo. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Zanzibar Saade Said Mbarouk alisema kuwa, mad...