NA KHAULAT SULEIMAN, PEMBA ZOEZI la uchukuwaji wa fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi za ubunge, uwakilishi na viti maalum linaendelea kupamba moto, kwa wanawake,wakiwemo wanahabari kupishana ofisi za CCM wilaya za kisiwani Pemba . Zanzibar leo kisiwani Pemba, ambalo limepiga kambi katika ofisi hizo, limeshuhudia wandishi wabahari wanawake, wajasirimali, watendaji wa serikali na waachama wingine, wakitekeleza haki yao ya kidemokrasia. Akizungumza na gazeti hili, mmoja kati ya watia nia hao kwa nafasi ya ubunge Jimbo la Chake chake, Ashura Abdalla Simai 'mabodo', alisema moja ya sababu iliyomsukuma ni kutekeleza haki yake ya kikatiba ya kisiasa. Alieleza kuwa, pindi vikao vya chama vikiridhia jina lake na kurudi, atakwenda bungeni kuwatetea wanawake wenzake na wingine, kwani walio wingi hawajafanya hivyo. “Wanawake wamekuwa wakikosa matetezi kwa kina, wa mambo yanayotuhusu, hivyo nimechukuwa fomu hii kujaribu bahati yangu kwa mara ya tano,”alisema. Afisa hab...